DOKEZO TRA kanda ya Temeke wananizungusha kubadili Tin location, uwajibikaji wao ni wa mashaka mno

DOKEZO TRA kanda ya Temeke wananizungusha kubadili Tin location, uwajibikaji wao ni wa mashaka mno

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Ofisi za TRA Temeke zote ni jipu la kutumbuka kabisa ninafatilia kuchange tin number location kutoka Temeke kwenda Ilala huu sasa ni mwezi wa tatu tangu tarehe 19/12/2025 mpaka sasa sijapata kufanikiwa

Nilianzia ofisi kuu ya kanda Temeke Banda la Ngozi pale nikazungushwa na online nimefanya kila kitu mpaka ID number nimepata nimeandika barua na imejibiwa kimbembe sasa kikawa kwa huyo ambae ndo anatakiwa amalize hiyo process yeye, aisee yule jamaa Mungu anajua la kumfanya amenikwamisha sana na sana hajawahi fanya hilo zoezi mwisho wa siku ananiambia nenda Mbagala ndo branch uliyosajilia

Nikaenda Mbagala nikafanya process upya ya kuandika tena barua cause online nilishafanya aisee nako Mbagala ni yale yale, huku sasa kuna mwanamke naomba mpaka kwenda kwa meneja nijue kwanini wananiambia tu kazi inafanyiwa lakini haiamishwi na kodi yangu ya pango la biashara inazidi kwisha bila biashara kufungua kwa ajili ya TRA Tanzania hawataki kuchange hii tin location.
 
Huduma kama hizi ni changamoto, kuna mazingira ya rushwa hapo yanatafutwa. Nakushauri kuangalia namna nyingine ya kufikisha kwa maboss wao, haiwezekani ufanye mchakato mpaka mwisho halafu wakuhamishie branch nyingine
 
Duuh Tin zinahama tena...si uko mkoa wa Dar es salaam au wenzetu huko kila wilaya ina operate tofauti japo ziko jiji moja
 
Duuh Tin zinahama tena...si uko mkoa wa Dar es salaam au wenzetu huko kila wilaya ina operate tofauti japo ziko jiji moja
Tumia pesa wewe acha kujifanya mzungu unayefuata taratibu,penyeza rupia acha longolongo
 
mimi nilizungushwa zaidi ya mwezi kuhamisha TIN kutoka Kigoma kuipeleka Arusha. yaani unawabembeleza TRA ili uilipe kodi Serikali!!!
 
Huduma kama hizi ni changamoto, kuna mazingira ya rushwa hapo yanatafutwa. Nakushauri kuangalia namna nyingine ya kufikisha kwa maboss wao, haiwezekani ufanye mchakato mpaka mwisho halafu wakuhamishie branch nyingine
Dahhh kabisa
 
Back
Top Bottom