pombe kali
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 282
- 561
Suala la kulipa kodi ni suala la kizalendo hii elimu inatakiwa iwe inawekwa kwenye mitaala ya shule zetu, mifumo yetu ya elimu imejikita zaidi kwenye kuajiriwa hivi majuzi imekuwa kama kauli mbiu ya serikali Kwamba watu wajiajiri kwani serikali haina ajira za kuwapa..inasikitisha sana inapotokea mmoja mbunifu anaamua kubuni Jambo lake kisha anajiajiri Anafikia mpaka hatua ya Kutoa ajira kwa watanzania wengine kitu ambacho serikali imeshindwa halafu Hawa watoza ushuru wanakuja kwa kuvizia kuvizia Mara wamfungie biashara yake au wamkamate na kumfungulia mashtaka ambayo ni Makubwa huwa najiuliza lengo ni kukatishana tamaa au kukwamishana kwani elimu hii ya mlipa kodi ingekuwa bure na inapatikana kiurahisi kungekuwa na haja gani ya kukimbizana na wafanyabiashara? Ukienda ofisi ya mapato kuna foleni na Huduma zisizoridhisha unaweza kushinda kutwa hapo utakuta unataka kuuliza nikitaka kufungua Duka natakiwa kuwa na vitu gani utaambiwa nenda kwa Huyu Mara Huyu, mamlaka ya mapato Mnakosa ubunifu na kututukanisha na serikali… wenzenu takukuru wameanzisha vilabu vya elimu kuanzia shule ya msingi nyie mnasubiri Mtu abuni biashara yake kisha mumvizie na kumfungulia mashtaka lengo ni nini?