Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Dhamira Ni hii[emoji116]Withholding Tax ni kodi anayolipishwa mpangaji kwa niaba ya mwenye nyumba kwa kigezo cha urahisi wa kuikusanya kupitia mpangaji! Na TRA ikimshauri mpangaji amdai mwenye nyumba ili amrejeshee alicholipa! Je, hili linawezekana? Hapana, huku ni kuporwa kwa kulazimishwa. TRA inapokuja na kauli tata kuwa mwenye nyumba alipie kodi ya jengo kwenye nyumba anayaishi mpangaji na huenda ni serikali ndiye mwenye nyumba! Utata mwingine, mpangaji atanunua umeme na kutozwa hiyo kodi, je serikali itamrudishia pesa yake? Na kama TRA inavyodai alipe mwenye nyumba kwanini isidai pia Withholding Tax alipe mwenye nyumba badala ya kumtwisha mzigo mpanganji?
Miaka miwili iliyopita niliwahi kuweka Post hapa ikihusu Withholding Tax kutozwa mpangaji lakini watu hawakunielewe, sasa kinachotokea ni kilekile tofauti ni majina tu kwani kodi zote mbili ni za jengo moja.Hii nchi tuishi tu hivi hivi.
Treatment/Collectability ya WHT on rental ina ukakasi sana, ni matokeo ya kuwa na wasomi wachache bungeniWithholding Tax ni kodi anayolipishwa mpangaji kwa niaba ya mwenye nyumba kwa kigezo cha urahisi wa kuikusanya kupitia mpangaji! Na TRA ikimshauri mpangaji amdai mwenye nyumba ili amrejeshee alicholipa! Je, hili linawezekana? Hapana, huku ni kuporwa kwa kulazimishwa. TRA inapokuja na kauli tata kuwa mwenye nyumba alipie kodi ya jengo kwenye nyumba anayaishi mpangaji na huenda ni serikali ndiye mwenye nyumba! Utata mwingine, mpangaji atanunua umeme na kutozwa hiyo kodi, je serikali itamrudishia pesa yake? Na kama TRA inavyodai alipe mwenye nyumba kwanini isidai pia Withholding Tax alipe mwenye nyumba badala ya kumtwisha mzigo mpanganji?
Tofauti na tozo za miamala, ambayo imekosa logic kabisa...kwa hili la LUKU nadhani mimi naweza kuwa na maoni tofauti.
Tukumbuke hapa lengo ni kuzifikia nyumba nyingi kadri iwezekanavyo, na kupitia mita za umeme nadhani imeonekana kama ni moja ya mbinu bora kwa sasa.
Nadhani kama yupo Mwenye ushauri mbadala wa jinsi ya kuzifikia Nyumba nyingi hata kama si zote basi atoe ushauri huo kwa Mamlaka.
Hili la kusema kwamba atalipishwa Mpangaji bado sioni athari zake kihivyo, unless kama ingekuwa kodi inalipishwa mara mbili...yaani Mpangaji na Mwenye Nyumba wote wanakatwa.
Sasa hata kukosa masikilizano kati ya Mwenye Nyumba na Mpangaji wake mnataka serikali ifanye nini? Kila nikijaribu kuitafuta logic ya Uma kwa kweli bado naona serikali wanashinda kwa pointi.
Kwa nini Nyie Wapangaji msiungane kuhakikisha mnarekebisha mikataba yenu na Wenye nyumba kuweka kipengele ambapo iwapo Mpangaji atakuwa anakatwa hiyo kodi bila Mwenye Nyumba kuhusika, basi mwisho wa mkataba Mpangaji atapunguza kiasi chote alicholipia Nyumba hiyo kwenye malipo ya mwishoni wa mkataba?.
Mimi warekebishe tu kule kwenye miamala ila huku kwenye Majengo sina shida, na ninaenda kulipa kabisa hiy0 12000 ili wasikate huku kwenye luku..12,000 kwangu imekaa haki kabisa.
Labda kama nitakutana na sababu nyingine zitakazonifikirisha tofauti lakini so far naunga mkono mfumo huo.
Najaribu kuelewa kiasi, ila bado naona kwa kuwa hakuna mbinu mbadala ya kurahisisha hili tupambane nalo mpaka likae sawa.Una mawazo sahihi. Nia ya serikali ni kupata tozo katika majengo wakiamini LUKU nyingi ziko kwenye majengo!
Sioni mpangaji au anayetumia LUKU akikwepa mzigo huu. Mlaji wa huduma ndio hulipa tozo na gharama zote. Wenye nyumba sasa wataandika mikataba itayoonesha au ongezeko la kodi kwa shiling 12,000 ili wakazilipe mara moja na zisionekane kwenye LUKU katika mwaka husika. Au kodi itabaki palepale na mpangaji kulipa kiasi hicho kupitia manunuzi ya umeme. Either way, hakuna net gain or loss kwa yeyote!!
Wasiwasi wangu ni kama hii inayoitwa tozo ya jengo imeunganishwa kwa kila kiwanja au jengo lililosajiliwa (ambalo linaweza kuwa moja kwa msingi wa hati kiwanja au hati ya ujenzi) au kila mita ya LUKU katika jengo hilo moja kuchukuliwa ni jengo in its own rights. Fikiria mita tano ambazo jumla yake kwa mwaka ni 60,000 na wapangaji watarajie mwenye jengo apunguze tu kiasi hicho kutoka koafi za wapangaji?? Katika baadhi ya sehemu katika nchi hii - hiyo ni sawa na kumpangisha mtu miezi kadhaa bure!! Itakuwa pia sio sawa kwa nyumba moja kulipa 12,000 na nyingine ya namna hiyo kulipa 60,000 kwa kuwa tu na idadi tofauti ya mita za LUKU.
Nadhani kuna kosa kuita tozo hii eti ni ya jengo. Ingeitwa ni tozo kama service charge ya kuwa na mita ya LUKU ingependeza. Sawa na ilivo kwa mita za maji au account benki ambapo kuna kuna tozo pia.
Nadhani kuna udhaifu katika messaging kwa upande wa serikali. Jambo hili hakikupaswa kuwa lilivokuwa!!