Wakuu, habari za mida hii. Nitashukuru kwa mawazo.
Nataraji kununua gari used ya biashara, Coaster, lakini mmiliki wake wa sasa hana karatasi yeyote kuonyesha alikuwa akilipa kodi ya mapato toka 2007 ambayo na hakika ni lazima uonyeshe kuwa uko up to date na kodi zao wakati unapotaka ku renew leseni ya biashara au hata usajili wenyewe wa gari, yani ku transfer kwenda kwenye jina langu. Yeye ana TIN namba yake, mimi sina, na sina deni na TRA.
Sasa nikienda TRA ku transfer jina huo mzigo wa kodi zake bado utaniangukia mimi? Nifanyeje.