TRA kukadilia kodi ya biashara yako kabla hujaanza?

TRA kukadilia kodi ya biashara yako kabla hujaanza?

wemode

Member
Joined
Aug 24, 2016
Posts
65
Reaction score
43
Mimi nina swali, kwanini TRA lazima uwalipe kodi kabla ujaanza biashara? wanajuaje utapata faida kiasi gani ndani ya mwaka?
 
Ata Mimi nashangaa wanachukua chao mapema kabla wewe ujajua changamoto
 
Ile kodi kimsingi ni makadirio kutokana na aina na asili ya biashara yako, eneo utakapokuwepo nk. Ukikadiriwa unalipia, lakini ikiwa mwisho wa mwaka hesabu zako zitakuwa chini ya makadirio uliyolipa, watafidia kwenye makadirio ya mwaka unaokuja MF kama ulikadiriwa laki 5 kodi, ukailipa ktk kipindi husika: utakapowasilisha hesabu zako Audited, ikaonekana ulitakiwa kulipa laki 3: basi ile baki ktk laki 5 yaani laki 2 wataipunguza ktk kadirio la mwaka unaofata , yaani ikiwa ni laki 5 tena, basi utalipia laki 3 tu.
Nadhani ni vema tu kulipa kadirio hata hujaanza ikupe mzuka wa kupigana kibiashara, pia itakusaidia ktk kuaminika kwenye ishu zingine...japo naona si lazima sana, MTU akishakadiriwa alipe kwanza: kwanini wasingoje ufanye ndio waje wakulipishe walichokadiriwa? Kuna wakati tulikuwa tinakadiriwa zero...sijui siku hizi
 
Muanzisha uzi, hukadiriwi kwa faida utakayoipata. Unakadiriwa mapato yako ya mwaka mzima kutokana na uasili wa biashara yako. Ila kuna kitu nimekuwa nikikiona wanachokifanya cha kipumbavu naweza kusema, huwez mkadiria mtu ukiwa umekaa tu ofisin, ingekuwa ni vyema wanakwenda kulitembelea eneo la biashara kwanza, waangalie upana wa biz yako ili muende sawa, ila wakati mwingine unakuta anakukadiria kwa namna anavyotaka yeye afisa yule kutokana na mazoea ya biashara ambazo amekuwa akizikadiria bila ya kujali vitu kama uwezo wa mtaji wako, mazingira unayofanyia biashara ile.
 
Niliwahi kuuliza hilo swali lako nikajibiwa, wengi walikuwa hawarudi kulipa tena baada ya kupewa TIN certificate ndio maana wanakomaa ulipe kwanza ili upewe ithibati ya kufanya biz kisheria. Ila mimi nikajiuliza tu, mwenye jukumu la kuhakikisha biashara zote zimesajiliwa kiutaratibu ni nan, niliuliza pia mamlakani, sikujibiwa
 
Hahahaaa hi I ukitaka kuwakwepa hawa jamaa Ni kuwadanganya mtaji wako na faida unayokusudia kupata
Vinginevyo unajikaanga na mafuta yako mwenyewe
 
Hivi kodi wanakadiriaje naomba kueleweshwa kwa mahesabu kabisa hili jibu litanisaidia namna ya kukabiliana nao hawa jamaa.
 
TRA wamegawa makundi kama mawili hivi ya walipa kodi za biashara kuna wale ambao wanapigwa kutokana na faida kwa mwaka hii ni kwa kund linalotunza records kama makampuni hivi na lile kundi lisilo tunza records hii zaid ni kwa wafanya biashara wale wa kawaida hawa hukadiriwa kodi kutokana na mauzo kwa mwaka... Mara nyingi wanaangalia eneo la biashara ilipo na wanaangalia na wafanya biashara wengine wa hilo eneo wanalipa bei gani na lengo la kulipa mwanzo ni utaratibu tuu wa kuhakikisha mapato yanakusanywa kwa uhakika na kwa wakati
 
Mimi nina swali, kwanini TRA lazima uwalipe kodi kabla ujaanza biashara? wanajuaje utapata faida kiasi gani ndani ya mwaka?
mimi nnachokijua kodi hukatwa kwenye income(faida) na huwa kodi inakatwa baada ya kukaguliwa vitabu vya kutoka kwa wakaguzi wa mahesabu(auditors) lakini kodi pia hukatwa kwa kuangalia mauzo yako(annual turnover) hii ni kwa wale ambao hawaandai financial statement, na mauzo yao kwa mwaka hayazidi 20 mill ........kwa hiyo hilo swala la kukatwa kodi mwanzoni ni jipya kidogo kwangu labda naomba ufafanuzi
 
Back
Top Bottom