Ile kodi kimsingi ni makadirio kutokana na aina na asili ya biashara yako, eneo utakapokuwepo nk. Ukikadiriwa unalipia, lakini ikiwa mwisho wa mwaka hesabu zako zitakuwa chini ya makadirio uliyolipa, watafidia kwenye makadirio ya mwaka unaokuja MF kama ulikadiriwa laki 5 kodi, ukailipa ktk kipindi husika: utakapowasilisha hesabu zako Audited, ikaonekana ulitakiwa kulipa laki 3: basi ile baki ktk laki 5 yaani laki 2 wataipunguza ktk kadirio la mwaka unaofata , yaani ikiwa ni laki 5 tena, basi utalipia laki 3 tu.
Nadhani ni vema tu kulipa kadirio hata hujaanza ikupe mzuka wa kupigana kibiashara, pia itakusaidia ktk kuaminika kwenye ishu zingine...japo naona si lazima sana, MTU akishakadiriwa alipe kwanza: kwanini wasingoje ufanye ndio waje wakulipishe walichokadiriwa? Kuna wakati tulikuwa tinakadiriwa zero...sijui siku hizi