TRA kukamata mizogo kwa ajili ya Efd machine ni kuonesha udumavu wa fikra zetu

Munjombe

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2018
Posts
2,107
Reaction score
2,985
Ukifika TRA unakuta na mizigo mingi sana kwa mfano TRA pale Longroom pamekua kama godwn la kuhifadhia mizigo,ukiangalia pale Kuna mizigo ya Congo,Rwanda,Burundi,Zimbabwe,Malawi,Zambia nk..ukiuliza wanakwambia hii ni mizigo tumeikamata haikua na Efd machine.

Nikamuuliza mmoja wao je hii mizigo ni magendo akasema hapana.Nikamuuliza mnajua Kuna mzimbabwe yupo alituma Dola zake apelekewe Mzigo wake?.

Jamaa confidently akajibu tunajua.Nikamwuliza unajua hapa Kuna watu wapo dukani mkoani huko wakiusubiri huu Mzigo?.Pia Nikamuuliza hii mizigo Huwa mnaibeba kama vielelezo mahakamani? Akesema hapana? Nilikasirika nikasema nyie ni wapuuzi kwa Nini uhangaike na Mzigo ambao sio ushahidi?.

Swali la Mwisho nilimwuliza ni kama hawaoni kama wanawakatisha tamaa wageni kuja Tanzania na kusababisha tukose wateja hao wanakuja kupunguza bidhaa za kichina na zetu na pia tunakosa pesa za kigeni akanijubu simple tu kuwa huo ndio utaratibu wao wa kazi.

Kwa mtazamo wangu naona hatuendi na wakati na tunatengeneza mianya ya Rushwa na ukandamizaji tu.Kwani usirekodi kosa na kuchukua maelezo na kuruhusu bidhaa ziende sokoni badala ya kurundika TRA na nyingine zinaozea pale tu.

Hoja ya Efd ni mfu kwa kwa machine sio kipimo sahihi cha mauzo na Wala sio kipimo Cha kipato.

I stand to be corrected.
 
Watu wafuate tu utaratibu hawatakumbana na mabalaa ya TRA. Sasa unasafirisha mafurushi makubwa bila risiti unategemea TRA wakufanyeje?
 
TRA wamekuwa wezi wa hadharani kwa kisingizio cha kuhakiki risit za EFD wanatumia kigezo hiko kudai rushwa

Haswa transpota ndio wanaokamuliwa inajulikana mzigo unalipiwa advance kwa ajili ya kusafirisha ukifikisha mzigo ndio unalipwa balance iliyobaki

Mfano kutoka Dar kwenda Arusha tani 30 inaenda kwa 1.5m advance ni laki 7 ukiwa na risiti ya laki 7 wanakataa wanasema hela ndogo wanakutishia kuandikia faini kubwa la sivyo uwape laki mbili

Huu ni wizi wafanyabiashara wanalalamika sana TRA wanaokagua risiti barabarani ni wezi na wala rushwa wakubwa
 
Na kwa nini hao hawatoe EFD?
 
Watu wafuate tu utaratibu hawatakumbana na mabalaa ya TRA. Sasa unasafirisha mafurushi makubwa bila risiti unategemea TRA wakufanyeje?
Umesoma mada ukaielewa?

Rudia kusoma mleta mada hatetei mizigo kutokuwa na document anachosema yeye kwanini baada ya kuonekana mzigo hauna risiti halali usiandikiwe maelezo kisha uruhusiwe kuingia sokoni au kwenda kwa muhusika?
 
hao wafanya biashara ndio wahakikishe wana document zote, sasa TRA itaaminije mzigo unaenda kulipiwa mwisho wa safari? Yaani ni vipi utawaaminisha? Mambo mengine ni ya kujitakia
 
Hapo tiyali ni kama Magendo, ni kesi nyingine
 
Sheria inasema hivyo?
 
Hapo tiyali ni kama Magendo, ni kesi nyingine
Kumbuka alihojiwa mfanyakazi wa TRA akasema hiyo mizigo wao hawaendi nayo mahakamani kama ushahidi bado so point ni ile ile wanashindwa nini kuandika maelezo ya mzigo husika kisha wakauachia?

Ni nini kimejificha hapa?
 
Badaye si wanazi dhulumu wanajipa wao....
Ndomana watu wengi wa TRA maisha yao huwa juuchini hapo badaye,maana wanaishi sana kwa dhuluma

Ova
 
hao wafanya biashara ndio wahakikishe wana document zote, sasa TRA itaaminije mzigo unaenda kulipiwa mwisho wa safari? Yaani ni vipi utawaaminisha? Mambo mengine ni ya kujitakia
Wewe umeona hawana documents mtu katoa risit inamaana hata invoice ipo hao TRA hawaelewi wanatakomalia rushwa

Au wewe ni mmoja wao unataka kutakatisha rushwa
 
Pande zote zina matatizo sio TRA sio wafanya biashara wala sio Serikali kote hovyo tu.
Cha msingi kama mfanya biashara ww jikamilishe ila ukitegemea mamlaka ziende sawa na ww na wafanyakaz walivyo na tamaa mh kaz ipo.
 
Nilimsikia mmoja anasema tutakufilisi, sijui kumfilisi mtu wanaona sifa...
 
Watu wafuate tu utaratibu hawatakumbana na mabalaa ya TRA. Sasa unasafirisha mafurushi makubwa bila risiti unategemea TRA wakufanyeje?
Mama upo jf karibu sana
Ila watendaji wako wanakuangusha sana.
 
Wafanyabiashara waache kulalamika napongeza TRA kwani wao wanataka kodi ya serikali kama utaratibu umekiukwa wakae mezani wamalizane.Nchi za wenzetu hii janjajanja hakuna
 
Back
Top Bottom