Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema imebaini uwepo wa magari barabarani yaliyobandikwa na kutumia namba ambazo hazijatolewa na TRA ama Taasisi nyingine za Serikali ambazo zimepewa jukumu hilo kisheria.
“Aidha, kumekuwepo na matumizi ya vibati vya namba vyenye rangi zisizotambulika kisheria vinavyowekwa mbele na nyuma ya vyombo vya moto (Plate number)”
“Hivyo, Wamiliki wa vyombo vya moto na umma kwa jumla wanatangaziwa kwamba, utengenezaji na matumizi ya vibati hivyo ni kosa kisheria kama inavyoelezwa kwenye Kifungu cha 8 cha Sheria ya Usalama Barabarani (The Road Traffic Act, 1973)”
“Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote anayekiuka sheria hii ikiwa ni pamoja na kutaifisha chombo cha moto husika”