Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 12,823
- 21,210
Nimejaribu kuisoma kanuni iliyotolewa na TRA ya kukokotoa kodi inayolipiwa bidhaa zinaoingizwa toka nchi za nje nimepata maswali mengi sana.
Mojawapo ya maswali ni kwanini Ushuru wa Forodha unatozwa Ushuru wa Bidhaa pia unatozwa Ushuru wa Ongezeko la Thamani (VAT)?
Kwanini Ushuru wa Bidhaa unatozwa Ushuru wa Ongezeko laThamani (VAT)?
Kwa kifupi hapa maana yake kodi inatozwa kodi nyingine kwa bidhaa hiyo hiyo moja. Hili limekaaje? Wabunge mko wapi mbona hamuhoji hii double and triple taxation?
Isome vizuri hiyo kanuni kwenye muongozo au ufafanuzi uliotolewa na TRA hapo chini. TRA tafuteni vyanzo vipya vya mapato siyo kodi zisizo rafiki kwa uchumi wa nchi. Panuaeni wigo wa walipa kodi msikamue toka kwenye bidhaa chache mnadumaza biashara na maisha ya walipa kodi.
Wananchi watashindwa kuagiza mashine au mitambo itakayo chochea maendeleo ya haraka na kuzalisha ajira nyingi.