TRA kwanini kodi (ushuru) hutozwa kodi tena kwa jina lingine? Wabunge mko wapi?

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
12,823
Reaction score
21,210
Nimejaribu kuisoma kanuni iliyotolewa na TRA ya kukokotoa kodi inayolipiwa bidhaa zinaoingizwa toka nchi za nje nimepata maswali mengi sana.

Mojawapo ya maswali ni kwanini Ushuru wa Forodha unatozwa Ushuru wa Bidhaa pia unatozwa Ushuru wa Ongezeko la Thamani (VAT)?

Kwanini Ushuru wa Bidhaa unatozwa Ushuru wa Ongezeko laThamani (VAT)?

Kwa kifupi hapa maana yake kodi inatozwa kodi nyingine kwa bidhaa hiyo hiyo moja. Hili limekaaje? Wabunge mko wapi mbona hamuhoji hii double and triple taxation?

Isome vizuri hiyo kanuni kwenye muongozo au ufafanuzi uliotolewa na TRA hapo chini. TRA tafuteni vyanzo vipya vya mapato siyo kodi zisizo rafiki kwa uchumi wa nchi. Panuaeni wigo wa walipa kodi msikamue toka kwenye bidhaa chache mnadumaza biashara na maisha ya walipa kodi.

Wananchi watashindwa kuagiza mashine au mitambo itakayo chochea maendeleo ya haraka na kuzalisha ajira nyingi.

 
Mkuu fanya biashara kwa akili ukianza fatilia haya mambo utafilisika au hutafanya biashara.
Sasa akili ya binadamu inataka kurahisisha mambo.
Hapa jambo rahisi kulifanya ni kukwepa kodi au kutoa rushwa. Je, nchi itaendelea kwa namna hiyo?
 
Sasa akili ya binadamu inataka kurahisisha mambo.
Hapa jambo rahisi kulifanya ni kukwepa kodi au kutoa rushwa. Je, nchi itaendelea kwa namna hiyo?

Fanya kwa akili wewe usilumbane na TRA , tumia akili kusurvive kwenye game
 
Mkuu fanya biashara kwa akili ukianza fatilia haya mambo utafilisika au hutafanya biashara.
Nilijua tuu kwamba lazima wajinga, narudia wajinga kama wewe mngeibuka. Nimekuita mjinga kwa sababu umeshindwa kuona rationale ya kinachojadiliwa hapa...
 
Du japo mmetoa mfano lakini naona maluweluwe
Gharama za mzigo wako:43,200,000
Kodi:26,892,000
43,200,000 + 26,892,000=70,092,000

Aisee wakwepa kodi wanakuwaga matajiri sana
 

Kwa nchi hii wewe staajabu ya Mussa:

Serikali isiyohitaji kodi haramu inaposhangilia mapato haramu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…