TRA madhara yenu kwa biashara ya utalii yatachukuwa mda mrefu kurekebishwa na huenda yasirekebishike kabisa

TRA madhara yenu kwa biashara ya utalii yatachukuwa mda mrefu kurekebishwa na huenda yasirekebishike kabisa

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,019
Reaction score
6,825
TRA Arusha mnakumbuka kesi hii
Mfanyabiashara wa usafirishaji na ukawala wa watalii alilipwa malipo ya mbele na watalii. Kabla ya watalii kufika likaja janga la Corona. Watalii wakafuta safari . Mfanyabiashara kwa uungwana akawarudishia wateja wake pesa zao zote ukiondoa gharama za banki. TRA kwa ubabe mkijificha nyuma ya sheria mkamlazimisha mfanyabishara alipe makato ya VAT. Mfanya biashara akajitetea wapi. mkamzimisha kwa kumtishia nakesi ya uhujumu uchumi. Hawa wako wengi- MMEUA BIASHARA ZAO. Kweli sheria ya VAT INASEMA HIVYO?! KAMA NI KWELI BASI ITAKUWA NI SHERIA YA HOVYO SANA NA KWA VILE NYIE NDIO WASHAURI WA SERIKALI KUHUSU MAMBO YA KODI NA NYINYI NI WA HOVYO.

Wengine kwa mashinikizo yenu walishindwa kuwarudishia wateja wao hela walizo tanguliza. Matokeo yake wameua uaminifu kwa wateja. Wao na Tanzania tunaonekana matapeli. Kujisafisha tuhuma ya utapeli tena kwa mzungu ni kama haiwezekani.
Kwa maoni yangu nyie TRA mme hujumu ROYAL TOUR kabla ikingali tumboni na mmeua utalii
 
Back
Top Bottom