TRA Mnatusababishia hasara Wafanyabiashara!.

Deus F Mallya

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2011
Posts
705
Reaction score
441
TRA kama taasisi ya serikali ya kukusanya mapato inapaswa kujua kuwa kupandisha kodi hovyo ni kuchelewesha maendeleo ya Taifa.

Pamoja na hayo, wafanyabiashara ndio watu walio Kwenye hatari kubwa zaidi ya kuanguka kibiashara (kupata hasara ) au kuingia kwenye migogoro ya kimkataba na wateja.

Kitengo cha kukusanya kodi Bandarini kwa maksudi jana kimetoa orodha mpya ya makadirio ya kodi za kulipwa kwa Magari yanayoingia nchini kutoka Japan. Mnafanya hivyo bila alert yoyote (japo hii si mara ya kwanza ) bila kujua mikataba yetu na Wateja ikoje. Ni ajabu kuongeza kodi kutoka 3.6 hadi 6.3 karibu 90%!.

Inawezekana mnafanya haya mkijua kuwa mna lengo zuri la kupunguza msongamano jijini Dar es Salaam au kuongeza pato la Taifa, lakini kumbukeni bila serikali kuhakikisha kuwa inauza zaidi nje kuliko kuingiza bidhaa ndani hata mkipandisha kodi kwa lengo la kuzuia bidhaa kuingia ni bure Kiuchumi.

Nimeandika logic ya kiuchumi leo na kuikabidhi kwa TRA. Naamini mtazingatia mapendekezo yangu.

Deus.
 
Serikali inabidi kuwa makini na mbinu zake za kuongeza kipato.Kuongeza Kodi kwa lengo la kuzuia Msongamano au kuongeza Kipato ni ufinyu wa kufikiri.

Kuna Mbinu nyingi za kuongeza kipato ambayo haihitaji kuongeza kodi bali kuongeza wigo wakukusanya mapato na Kuongeza miundombinu kama barabara,usafiri wa umma kuwezesha watu kufika kwa wepesi maeneo mbalimbali na si kuongeza kodi ya magari.

Hali hii itachangia pia kufukuza wateja ambao wamerejea kuitumia bandari yetu baada ya mabadiliko ya hivi karibuni.Serikali pia itawavunja moyo na kuwarudisha nyuma wafanya biashara ambao wameweza kujiimarisha na kutoa upinzani kwa wafanya biashara wa nje jambo ambalo ni jema kwa ustawi wa nchi hii.

Naiomba serkali sikivu iwasaidie wafanya Biashara badala ya kuwadidimiza.
 
Nimeshauliza mara nyingi humu,kwanini bidhaa Uganda ni bei rahisi sana! kuliko Tanzania wakati waganda hawana bandari?
hata petrol na disel ni bei rahisi kulliko dar.
Tanzania inakuwa soko la bidhaa za nchi za east African.
mkuu deus nisaidie hili
 
Hata magari uganda ni bei rahisi mno!
 
Tanzania tumeishiwa mbinu za kukusanya mapato,tunashindwa hata na nchi ambazo mda mwingi wapo kwenye vita.Mabadiliko ni mda muafaka sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…