Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Ninatambua kwamba ni wajibu wa mfanyabiashara yoyote kulipa kodi ili kuchangia pato la Taifa na hatimaye kuwezesha maendeleo, na ninaunga mkono jambo hilo.
Lakini Kodi inapaswa kulipwa kutokana na kinachopatikana kwenye biashara husika na si vinginevyo.
Lazima tukubali kwamba ujenzi wa mabarabara na miundo mbinu mingine kama mitaro mikubwa unaochukua muda mrefu sana, unaathiri kabisa biashara za watu mitaani, kwa mfano, Ujenzi wa barabara ya mwendo kasi ya Chang'ombe inayoanzia JKT kupitia chuo cha ualimu Duce, Keko hadi VETA, ujenzi ulioambatana na Mtaro mkubwa sana wa Maji unaoelekea baharini umeua kabisa biashara za watu kwenye eneo hilo lenye barabara nyembamba isiyo na Plan B, kwa miaka mitatu mfululizo ni mitaro na ujenzi usioisha.
Uchunguzi wangu umebaini kwamba zaidi ya 75% ya wateja wa biashara zilizo pembezoni mwa barabara ni wapita njia, yaani ni wenye baiskeli, pikipiki na Magari, sasa ujenzi wa muda mrefu wa barabara hizo umeathiri moja kwa moja mapato yao, kuwadai kodi yoyote watu hawa ni sawa na kutaka kuwadhalilisha tu, watalipa nini kutoka wapi? Kwa miaka mitatu ni mitaro mikubwa mbele ya ofisi zao, watapata wapi hela hawa?
Hata sisi tulio kule Mbozi road kwenye viwanda na Magodown tayari tumeanza kukiona cha moto kwa kufungwa kwa Barabara ya VETA tu, hakuna gari inaingia wala kutoka kwa kupitia barabara hiyo kwa miezi lukuki sasa, hivi tunawezaje kusafirisha mizigo yetu mikubwa na mizito, yakiwemo masink na Tiles kupeleka kwa wateja wetu ili tupate hela?
Hatupingi ujenzi wa miundo mbinu maana ni maendeleo, lakini tunashauri TRA na hizi Halmashauri ni lazima ziwe na utaratibu Maalum wa kodi na leseni kwenye maeneo ya namna hii, vinginevyo mtamfunga kila mtu, Mitaro miaka mitatu mbele ya ofisi zao wanawezaje kusurvive hawa?