Scaramanga
JF-Expert Member
- Aug 19, 2020
- 490
- 704
Nimepokea ujumbe toka kwa viongozi wangu wa biashara kuwa jumatatu tunatakiwa tusifungue biasharaeneo la kariakoo. Nimeuliza wenzangu wameniambia kuwa tra juzi walitoa maelekezo ya kujisajili stoo tunazomiliki, kama mtu unayo stoo ya kuhifadhia bidhaa za biashara.nimempigia jamaa yangu kumuuliza kulikoni huko tra kanijibu kuwa ukweli siyo kwamba kuna kulipa kodi kilichopo ni usajili wa stoo hakuna kodi mpya.nimerudi kwenye jumbe nazopokea kuuliza viongozi wanasema ni kodi.sasa nashindwa elewa kama tra wao wanasema siyo kodi ni usajili viongozi wangu mmetoa wapi hii maana nyote kwangu mimi mfanyabiashara nawategemea.nikajiongeza nikapiga hadi simu tra kituo chao cha simu na maswali wameniambia hakuna kitu kama hicho kilichopo ni usajili wa stoo na siyo ulipaji wa kodi.mimi kiukweli ninafamilia inanitegemea na biashara yangu ndiyo mkombozi wangu katika kuishi.nahofia nikifunga biashara yangu nitoe wapi pesa ya kula. kama kusajili tu stoo sioni kama kuna shida mimi nilidhani ni kulipa kodi mpya.