Wana JF,
Nimekuwa nikipata taabu kidogo na kadhia ya TRA wakati wanapokuja na mdali wao kufunga vibanda kwa ajili ya kukusanya Tzs.60,000/= za kodi na pamoja na faini ambayo ni Tzs. 35,000/= zote hulipiwa benki. Tatizo langu kiufundi ni kwamba biashara hizi ni ndogo ndogo na kimfumo kodi inatakiwa kulipwa mara baada ya kufunga hesabu za fedha kwa ufahamu wangu.
Kitendo kinachonishangaza ni kwamba hata kabla mwaka husika wa fedha haujaisha wao wameshakusanya kodi yao sijui hapa wanatumia vigezo gani hasa nazungumzia pia biashara za boda boda, bajaj ama taxi. Najaribu kufanya ulinganifu na makampuni makubwa ambayo sitapenda kuyataja hapa ambayo ukiondoa PAYE na NSSF wanaweza wasilipe kodi kabisa kwa sababu ya hasara katika biashara!!!! Kama wapo humu watuambie wanatumia fomula gani kupanga kodi ya vibanda bila kuangalia jiografia ya mji ama wilaya ama kitongoji pia.
Kitendo cha kufunga makufuli katika kibanda cha mtu mpaka kodi na faini ilipwe kabla ya mwaka wa fedha wa mfanyabiashara husika kuisha je ni halali ki sheria? kama wanasheria wamo humu watupe mawe ili turuke nao mahakamani tulambe fweza za madai wametufika kooni hawa, kufunga kibanda cha mtu si jinai? PASIPO AMRI YA MAHAKAMA....hapa ninaomba ushauri....!!!