TRA na ushuru wa used cars

Konzogwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2008
Posts
434
Reaction score
156
Habar wakuu! Nisaidieni kujua hili, TRA hutoza ushuru kwa bei ya kununulia gari tu au ni pamoja na ile ya kusafirishia?...mfano mimi nahitaji kununua toyota vitz toka japan kwa us& 511 halafu c&f to dar es salam nimeambiwa us& 1700.
Nliwah kusikia kuwa kwa gar lenye umri kuanzia miaka 10 ushuru ni asilimia 80. Sasa swali langu la msingi ni kuwa, hiyo 80% ni kwa bei ya gari tu au ni pamoja na shipping cost?
Natanguliza shukrani.
 
Hyo vitz unaendesha wewe au unaonga? Kama ni wewe ebu badili gari bwana mwanamme na vitz wapi na wapi?
Hebu tujaribu kuwa serious humu JF vinginevyo ujinga (ignorance) wetu aliousema Mwalimu Nyerere tutakufa nao; unadhani kuendesha mgari mkubwa ndiyo ujanja! Nenda na wakati ili ujinga ukutoke.
 
Hyo vitz unaendesha wewe au unaonga? Kama ni wewe ebu badili gari bwana mwanamme na vitz wapi na wapi?
Vitz is my favourate car also! Tofauti ya mark II yako na vitz yangu ni nini. Wote tunafika tunakotaka kwenda na zaidi ya yote mahali ambapo wewe utatumia lita tano kufika mimi mwenzako nitatumia lita mbili na nusu. Nani mjanja? Au kuwa mwanaume ni kuwa na matumizi makubwa?
 
Wadau wengi hamjamsaidia muuliza swali. Badala ya kumueleza TRA wanacharge vipi ushuru, mmejikiza zaidi katika kujadili aina ya gari.
Mkuu TRA wanacharge CIF (ambayo ni bei ya kununulia pamoja na usafiri)
 
kwa ufupi ushuru unatozwa baada ya kujumuisha Cost (gharama ya gari) Freight (shipping cost) na Insurance. yaani CIF TANZANIA

MFANO UMENUNUA GARI DOLA 500, FREIGHT DOLA 1000. UNAJUMLISHA HALAFU UNAZIDISHA X 1.5 % UNAPATA INSURANCE.
500+1000=1500X1.5 % =22.5
KWA HIYO UNAJUMLISHA ZOTE HIZO 500+1000+22.5=1522.5 HII SASA NDIO CIF YA GARI YAKO AMBAYO TRA WANAZIDISHA MARA 80 % jawabu 1218 USD ndio ushuru wenyewe. zaidi nitwangie 0714229040
 

Achana hizo ukiingia kwenye web site ya TRA tafuta kitu Tax Estimator au ingia hapa Welcome to GariYangu.com - GariYangu.Com
 
Hebu tujaribu kuwa serious humu JF vinginevyo ujinga (ignorance) wetu aliousema Mwalimu Nyerere tutakufa nao; unadhani kuendesha mgari mkubwa ndiyo ujanja! Nenda na wakati ili ujinga ukutoke.

Pole kama unaendesha vitz,duet,starlet,raum,suzuki jimny,hivo vigari ni vya mademu tu mwanamme na midevu plus mip**mbu unaedesha vitz???
 
Achana hizo ukiingia kwenye web site ya TRA tafuta kitu Tax Estimator au ingia hapa Welcome to GariYangu.com - GariYangu.Com

Wewe ni MBUMBUMBU KABISA, Kwa kifupi watanzania asilimia 99 wenye magari pamoja na wewe unaejiita mwanamume wanatakiwa kuendesha magari ya aina hii, kujikweza sio maendeleo weeeeeeeeeeeee kwa kifupi ni MWIZI sio mhangaikaji ndio maana unamcheka anayetaka kununua Vitz.
 
Pole kama unaendesha vitz,duet,starlet,raum,suzuki jimny,hivo vigari ni vya mademu tu mwanamme na midevu plus mip**mbu unaedesha vitz???

Mkuu King Kong III leo umeniacha hoi sana, coz kuna jamaa yangu anaendesha raum amejiskia vibaya sana hapa. Vipi Corolla je?
 
Last edited by a moderator:
Utakuta King Kong ana siti yake kwenye DCM la mbagara humu ana discourage wenzake tu
 
Mkuu kauliza swali hili nyie mnajibu hili, mi nilikuwa naendesha na namiliki chevlolet station wagon niliyokuja nayo toka ughaibuni kwa mara ya kwanza niliona ufahari kuendesha gari kubwa lakini kadri muda ulivyokuwa unaenda nikaona ni ujinga kutokana na foleni kwani gari ilikuwa inakula mafuta balaa nikabidi ninunue toyota duet hadi leo naifurahia sana kwa ulaji wa mafuta hapa town na hizi foleni
 

kama huelewi kusoma kaa kimya! nimekwambia ingia website ya TRA au Welcome to GariYangu.com - GariYangu.Com sijashauri asinunue. acha us**ge wewe! au umeingiziwa nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…