TRA - Napasuwa Ufisadi Mwingine!

kupata ushahidi kirahisi ni ngumu, lakini kama kuna ufisadi, ilikuwa ni kazi ya serikali kuzisaka hizo documents kwa sababu wananchi tayari wameshatoa wasiwasi wao upo kwa nani.

lakini hilo tuote tu kwa kuwa halitotokea hapa tanzania katika miaka hii ya karibu.
anaetishia kuwafichua mafisadi anakufa taratibu , na habari tunapewa wiki baada ya kufa
 


Nakubaliana na wewe baadhi ya maeneo kama vile kudai pesa maeneo mengi yawe ya serikali kuu au hata serikali za mitaa lakini kwa suala la majambazi hilo nakukatalia kwa sasa limepungua sana maan mara yangu ya mwisho nakumbuka majambazi ambao wameripotiwa ni wale ambao wamekuwa wakibia wateja katika nyumba za kulala wageni tu kwa kuwavizia huko wakati wamelala na si vinginevyo tofauti na ilivyokuwa hapo awali wakati majambazi yalipokuwa yameshika hatamu yalikuwa yanaweza kupora machana kweupe yaliweza kupora kwenye maduka ya kubadirishia na kufanikiwa kutoroka bila ya kukamatwa
 

JE INAWEZEKANA SAID MWEMA AMEKUSIKIA SOMA HAPA CHINI....

•Mabadiliko makubwa Polisi, Tibaigana ang'atuka

*Kova achukua nafasi yake, Rwambow aenda Mwanza

Na Reuben Kagaruki

JESHI la Polisi limefanya mabadiliko makubwa katika safu yake ya uongozi kuanzia ngazi ya wilaya, mikoa na wakuu wa upelelezi kufuatia maofisa wake wengi kufikisha umri wa kustaafu kwa lazima ifikapo Julai 1, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Said Mwema, Kamishna wa Utawala na Fedha, Bw. Clodwig Mtweve, alisema Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Alfred Tibaigana anastaafu na nafasi yake inachukuliwa na Bw. Suleiman Kova, aliyekuwa Mbeya.

Atakayeziba nafasi ya Bw. Kova ni Kamanda wa Mkoa wa Bw.Stephen Zelote ambaye nafasi yake inachukuliwa na Bw. Jamal Rwambow, akitokea Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni.

Alisema Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Bw. David Saibullu anastaafu na nafasi yake inachukuliwa na Bw. Liberatus Lyimo Barlow, ambaye kabla ya uteuzi huo, alikuwa Ofisa Nadhimu Utawala na Fedha Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Aliyeteuliwa kushika nafasi ya Bw. Rwambow Mkoa wa Kinondoni ni Bw. Mark Kalunguyeye, ambaye kabla ya uteuzi wake alikuwa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Bw. Ray Karama, aliyekuwa Kikosi cha Kutuza Ghasia, Dar es Salaam ameteuliwa kuwa Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Wezi wa Mifugo Makao Makuu Arusha.

Bw. Mtweve alisema, Bw. Abdallah Msika amehamishwa kutoka mkoani Kagera na kupelekwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam huku ASP Salewi aliyekuwa Kamanda Mkoa wa Pwani akipelekwa kuziba nafasi yake.

Mabadiliko hayo pia yamemgusa Bw. Mwakyoma aliyekuwa Makao Makuu ya Polisi na sasa anaenda kuwa RPC Mkoa wa Pwani huku RPC wa Tabora, Bw. Mshahili akirejeshwa makao makuu Dar es Salaam na nafasi yake kuzibwa na Bw. Emson Mmari, aliyekuwa Makao Makuu ya Upelelezi.

Bw. Lucas Kusima aliyekuwa Baraza la Ulinzi na Usalama, amehamishiwa Makao Makuu na nafasi yake itazibwa na Bw. Brown Lakey kutoka Makao Makuu ya Upelelezi.

Katika mabadiliko hayo pia yamewagusa wanawake wawili ambapo Bi. Marry Nzuki aliyekuwa OCD Mkoa wa Dodoma anakwenda kuwa Kaimu Kamanda wa Polisi TAZARA huku SSP Lucy Makelemo aliyekuwa OCS Uwanja wa Ndege Mwanza anakuwa Staff Officer I Dar es Salaam.

Alisema mabadiliko hayo pia yamewagusa wakuu wa upelelezi wa mikoa Mara, Kigoma, Shinyanga na Mbeya. Wanaotarajia kustaafu nafasi zao zimechukuliwa na Bw. Msato Marijani aliyekuwa OCD Wilaya ya Biharamulo (Kigoma), Bw. Deusdit Kato (Mara). Kabla ya hapo alikuwa OCD Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam.
 
Labda tuanze mkakati wa kuwachoma moto hawa jamaa kama wa south wanavyowafanyia unyama ma black wenzao. Tuwatokomeze hawa jamaa waishilie mbali. Kuna haja ya kuunda Mungiki ya Bongo. Hali hii inakera saaana, na inatuumiza mno!

Kweli zaidi ya hapo hakuna kwani serikali yetu ipo nao kwa sasa. Wanawaficha hawa mafisadi. Kwa mfano, huyu saidi mahonda akihisi tuu kuwa umemuibia katika maduka yake anakufungia ndani ya store na kuanzan kukupa mkong'oto yeye na ndugu zake. Wameshamfanyia kijana mmoja alikuwa akifanya kazi kwao, halafu wakamweka ndani, ufisadi ni hatari kweli, yaani hu8yo kijana wamempiga halafu wakamweka ndani sijui siku ngapi, kawekwa pale kituo cha polisi Msimbazi bila kufikishwa mahakamni na mwisho wakamwachia kwa kula mateso na wazee wake wakasema wao watalipa hizo tuhuma kwa kulipa wanachosema kaiba. Yaani hakufikishwa mahakamani kwa masiku tele na Said Mahonda kuwa vituo kama vya msimbazi anavimiliki, pesa anazogawa huko zinatosha kufanya asishikwe na aweze kumuweka au kumtowa ndani yeyote yule kwa kosa lolote lile.

Hata mdogo wake kwa Jina la Abdallah, alisha mvunja mkono mtu kwa kudhani kuwa kaiba dukani kwao na hata baada ya kupelekwa kituo cha Msimbazi hakuna alichofanywa na badala yake yule alievunjwa mkono ndio kawekwa ndani kwa kubambikizwa, huyo huyo ndugu yake alishikwa kwa kutowa bastola hadharani, akawekwa Msimbazi wakala fedha wakamwachia. Jamani Serikali iko wapi? mna kula kiasi hamjali hata raia zenu masikini kwa ajili ya ufisadi na kushirikiana na mafisadi?

Hebu wale wema kidogo na mlio kwenye madaraka na mnapitia humu, fuatilieni hizi habari kwa manufaa yetu.
 
Hatari, sasa wazee wa kulindana wataanza kuteteana,ohh hakuna ushaidi ni tuhuma tu! weka mambo hadharani waone aibu kama mzee wa container terminal!
 
Hii ingali ipo katika malumbano? Kuna hatua zozote zimeshachukuliwa?
 

Habari hii iliwahi kuandikwa kwenye Gazeti la Raia Mwema wiki chache tu zilizopita!! Kumbe ni stori ya siku nyingi sana!!!

TRA ilimeshaidia watu wengi sana kutajirika haraka haraka: ama wafanya biashara au waajiriwa wa TRA. Kama ambavyo law of conservation of energy inavyofundisha, utajiri unaotokana na TRA ni husibababisha serikali kukosa mapato yake tena kwa kiasi kikuba sana, jambo ambalo huchangia serikali yetu kushindwa kujitegemea.
 
Wakuu zangu hivi nyie ndio leo mnayajua haya? mbona ni NDIVYO ILIVYO kwa sisi kina NDIVYO TULIVYO?..mchezo huu upo miaka wala sii huyo peke yake, matajiri woote wanaingiza fedha zao huko na siku hizi wanafungua storage za container ambazo wanakawiza makusudi kutoa mizigo ili mteja alipie gharama za storage. It's a big business kiasi kwamba mizigo mingi ya kwenda nchi za nje hasa Kongo na Rwanda zinapitia Bandari ya Mombasa. Zanzibar nako mchezo tayari umeingia...Ndio Bongo...
 
Nchi yetu kwisha habari yake kumbe hizi news ziko siku nyingi..
Nilizisoma juzujuzi Raia Mwema..kumbe hata hiyo kamati iliyoundwa na bodi ya TRA ni geresha tuu
hayo mambo yanajulikana toka zamani..kwanini wasichukue hatua??? wanawaogopa au wako katika payroll???
Taifa halitatoka kwenye umaskini kama tuteendelea kufumbia macho watu wachache kwa Fedha za magumashi...
 


the only way to clear up this madness is thru assassination ..... i am serious ningekuwa kiongozi ningetengeneza kundi flani la searial killers kwa ajili ya maslahi ya taifa... nikiona kuna mgogoro mkubwa ambayo kisheria hautotupa haki kama taifa... tunamuua huyo fisadi na kundi lake na kuwaacha wengine wajue bila ya kua na ushahidi ili wajue kula NATIONAL SECURITY HAS ITS PRICE... kama wao wanatunyonya na hatuna ushahidi wa wazi na wao tunawaua huku wakijua na bila ya kuwa na ushahidi wa wazi...
 
mmmhh, mtabaki hivyo mlivyo kunung'unika kwenye majarida huku mali zenu zikisombwa, mkiambiwa fanyeji mabadiliko ya system hamtaki ndo kwanza mnakuwa na vihelehele vya kuwachangia watu waende wakachukuwe forms za kugombea tena uongozi, unafikili serikali iliyoimara itafanya upuuzi kama huo? angalia mataifa ambayo leo hii yamepiga hatua ktk uchumi duniani kama yanaendekeza ujuha huu, nini faida ya kuwa na wasomi katika nchi? mikataba mibovu ni yetu, umasikini ni wetu, siasa chafu na zisizo na tija ni zetu, viongozi vihiyo ni wetu, mafisadi ni wetu, hakika nasema Taifa hili kuendelea ni mpaka kizazi hiki kiishe kwanza ktk uso huu wa dunia na kianze kizazi kingine, inatia hasira sana hakuna rasilimali utakayouliza ktk hii nchi ukaambiwa haipo, kila kitu kipo, tuna mali asili nyingi na zenye faida, lakini kwa upeo mdogo na masilahi binafsi ya watawala wetu wanathubutu kuwekeza hata kwenye kuwinda swala tena wanapewa waarabu, huu ni umasikini wa mawazo, na kukosa mipango makini, mtaji kiasi gani unaohitajika kuwinda? mimi natamani kilichobaki kwa sasa ni popote alipokiongozi anayetukwaza ni kuhakikisha watu wanajitoa mhanga tu basi, huu ni upuuzi tena wa hovyohovyo, kila mwaka tunaambiwa uchumi wa taifa umependa kwa asilimia sufuri nukta kadhaa, watu wanakula hela za mapato ya nchi tena bila hata haya, ni sekta ipi yenye unafuu? kote uozo utupu. KONTENA imekamatwa ughaibuni ikiwa na shehena ya mali asili zetu mpaka leo kimya! waziri wa utalii anacheka tu, TICTS uozo mtupu nini kinafanyika kama si ujinga mtupu, Reli ndo kabisa ni bora hata watu wakatembea kwa miguu kuliko huo upuuzi , IPTL, RICHMOND, MEREMETA, nk nini kimetokea kama si kuwakejeli watanzania, inanifanya niaamini ndani ya Tanzania kuna nchi nyingi, hivyo ni ngumu kufikia maendeleo. katiba yenyewe ni butu tena kibogoyo, sheria za nchi zimefanywa kama verse za nyimbo tena soft songs a.k.a R&B, kiasi kwamba hata mafisadi wanazipenda kwani zinawambembeleza na kuwaletea usingizi mnono, kila kukicha ushahidi haujakamilika! hao wanaochunguza wanataka tuamini nini sasa? kwamba kazi imewashinda ama? upelelezi gani unaochukuwa zaidi ya miongo kadhaa? mwisho unaambia mashahidi waliotakiwa kuja kutoa ushahidi walishafariki, hizi ni janja zao tu, wanabaki kuhukumu kesi za wizi wa kuku, bata, mbuzi. akina Endrew chenge wanaendelea kunywa whisky tu kana kwamba hawajafanya lolote baya, siku watanzania wenye nia ya kweli watakapoamka toka kwenye usingizi mzito ambao umewapitia miaka mingi sasa, ndipo hapo tanzania itakapo endelea vinginevyo ni mazingaombwe tu
 
Duh, kumbe hii habari ni ya siku nyingi? Vyombo vyetu vya usalama vimelala usingizi fofofo. Wangeliifanyia kazi tungeliweza kuokoa mabilioni.. ah, --- au zingetumika kwenye safari za mzee na mama??
 
Hapa ndipo quality ya JF inapojiweka wazi yenyewe. Nchi yetu haina mlinzi, wananchi wakijitolea kutoa habari hakuna anayeziamini wala anayeshinikiza uchunguzi. no more to be done ni kuganga maisha tu sasa.
 
Hapa ndipo quality ya JF inapojiweka wazi yenyewe. Nchi yetu haina mlinzi, wananchi wakijitolea kutoa habari hakuna anayeziamini wala anayeshinikiza uchunguzi. no more to be done ni kuganga maisha tu sasa.

Tangu 2008 habari zilishawekwa wazi..... leo ndio wanajifanya kuunda tume???? Agrrr
 
Hats off to JF. Nimeisoma hii habari majuzi tu kwenye gazeti la Raia Mwema kumbe wakuu walishaimwaga humu 2008! Basi tukubali tu kuwa kwa kadiri tutakavyoendelea kuubeba utawala huu tusitegemee jipya zaidi ya nchi kuendelea kuliwa na wahuni hawa wa kiwango cha chini hasa.
 
JF endelea kuishi tu hizi sarakasi zinazofanyija sahivi zilishajadikiwaga kitambo
 
Angalau hata kapicha,ili na sisi wa huku Bwendanseko tumuone anafananaje...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…