TRA punguzeni foleni zisizo na maana

TRA punguzeni foleni zisizo na maana

mjarrab

Senior Member
Joined
Nov 13, 2015
Posts
108
Reaction score
55
T.R.A PUNGUZENI FOLENI ZISIZO NA MAANA

Hakuna sababu yoyote ya Maana ya wamiliki wa magari ya biashara kwenda TRA kupanga foleni kwa ajili ya Makadirio ya kodi za Mapato. Magari yote yanaeleweka na kazi zake zinaeleweka.

Mfano kwa magari ya Mizigo ya ndani yatozwe kodi kulingana na uwezo wa tani zake za kupakia. Kila gari itozwe kwa uwezo wa tani zake. Kwa mfano kila uwezo wa tani 1 utozwe kodi ya sh Laki 1 kwa mwaka. Ikiwa gari yako ya Mizigo ni tani 3.5 utalipia Laki 3.5.

Kwa kuwa yapo magari yanayopakia tani zaidi ya uwezo wake mfano fusso,watu hao wapewe fursa ya kujichagulia wenyewe kwamba gari zao zibebe mwisho mzigo kiasi gani. Kile kiwango atakachojichagulia ndicho atozwe lakini kisiwe chini ya uwezo halisi wa gari. Ikiwa atachagua kupakia tani mpaka 10 atalazimika kulipia sh Milioni 1 kwa Mwaka.

Na uwekwe mfumo wa kudhibiti katika mizani ambao unatakiwa uoneshe kiwango cha gari ilichoruhusiwa kubeba, ikiwa limezidi kiwango cha uwezo Basi litozwe ongezeko la tani zilizo zidi.

Magari yote ya Mizigo kupitia kadi za usajili yanaonyesha sifa zake, mmiliki wake,uwezo wake wa kupakia n.k. na taarifa zote kuhusu sifa hizo zipo T.R.A.

Sasa hakuna sababu za kwenda kuweka foleni TRA uwekwe mfumo wa kulipia kwa njia ya simu Kama ilivyo kuwa kwa malipo ya Motor vehicle huko nyuma kabla ya kuondolewa.

Hii itaondoa usumbufu na kuondoa malalamiko wa ubambikizwaji wa kodi,na kuondoa rushwa kwa sababu itakuwa hakuna sababu ya kukutana na Maafisi ambao hutumia Makadirio Kama nyundo ya kutengeneza njia ya kujipatia rushwa.

Pia ipo njia nyingine ambayo ni rahisi zaidi na isiyo na gharama Wala usumbufu. Gari zote zinatumia mafuta ukiweka sh 100 kwa kila lita ya Mafuta,na mia kwa kila kilainishi(oil) hakuna atakae kwepa kulipa kodi automatically anaefanya kazi zaidi atatumia mafuta zaidi na atakuwa amelipia kodi zaidi hivyo kutakuwa na aina fulani ya haki.

Mfano coster inayo tumia lita 10 tu kwa siku itakuwa imechangia sh 1000 Kama ni Sehemu ya kodi ambapo kwa mwezi ukitoa siku za service wastani wa sh 25,000/ kwa Mwaka atakuwa amelipa sh Laki 3.

Hii ni Coster ya kiwango cha chini,lakini zipo zinazo tumia hadi lita 20-30 inamaana watakuwa wamelipia zaidi laki 6-9 kwa Mwaka.

Yapo malori,mabasi,ya safari ndefu, tuchukulie mfano Basi 1 kutoka Dar- Dom tukadirie kiwango cha chini ni lita 100. ina maana ni sh elfu10 inapatikana kwa safiri moja tu ya kwenda Dom kwa siku kwa Basi moja. Kwa Mwezi hazipungui tripu 20 hii ina maana ni laki 2 na kwa Mwaka inakuwa mil 2.4.

Hiyo ni Basi ya kwenda Dodoma. vipi ikiwa mwanza,kahama shinyanga n.k serekali itaingiza mapato kiasi gani?

Na uzuri wa njia hii ni kwamba Serekali itatachukua pesa yake kwenye makampuni ya Mafuta kabla mafuta hayajaingia sokoni.

Wenye vyombo vya usafiri wakieleweshwa kwamba mia hiyo ilio ongezeka ni kodi hivyo hawataruhusiwa kuongeza nauli katika magari.

Uzuri wa njia hii hata boda boda anae tumia lita 1 kwa siku atakuwa amechangia wastani wa Elfu 24 kwa mwaka.

Magari binafsi nayo yatakuwa yamechangia kwa kiasi kikubwa!.

Serikali itakuwa imesha chukua pesa yake mapema Bila usumbufu na gharama katika ukusanyaji wa kodi.

Maoni yangu yanaweza kuwa na Mapungufu.
Ila Serikali iangalie mfumo rafiki wa ulipaji kodi kwa njia nyepesi kwa kupunguza secta ya Usafirishaji ipungue katika foleni za T.R.A.

Foleni za T.R.A ndizo zinazoleta, Usumbufu, kero, Mazingira ya Rushwa n.k.

Hivyo njia bora ni kuangalia njia bora za kuondoa janga hili.
 
Nadhani utaratibu mzuri zaidi ulikuwa ni huu wa kutoza kodi za magari per litre na kuondosha kabisa masuala ya makadirio.

Kwa hapo magari ya biashara automatically yatakuwa yanalipa zaidi kulingana na umbali yanayokwenda kwa siku na mizigo yanayobeba.

Kodi ya 50/= @ liter kwa bus la kutumia liter 300 kwa siku kwa mfano ni 150,000/= hizi ni pesa ngapi kwa mwaka? Makadirio ya nini tena hapo?

Yale yale ya Road Licenses poorly administered kama ilivyokuwa awali.

Siyo siri TRA imejaza watu mizigo wasiokuwa na tija yoyote.
 
Nadhani utaratibu mzuri zaidi ulikuwa ni kutoza kodi za magari per litre na kuondosha masuala ya makadirio.

Kwa hapo magari ya biashara automatically yatakuwa yanalipa zaidi kulingana na umbali yanayokwenda kwa siku.

Kodi ya 50/= @ liter kwa bus la kutumia liter 300 kwa siku ni 150,000/= hizi ni pesa ngapi kwa mwaka? Makadirio ya nini tena hapo?

Yale yale ya Road Licenses poorly administered kama ilivyokuwa awali.

Siyo siri TRA imejaza watu mizigo wasiokuwa na tija yoyote.
Kabisa!!
 
Kodi ya mapato inakatwa kutoka katika pato alilopata mtu (mfanya biashara) ambapo magari ya biashara ni mojawapo.
Sasa kodi ikiwekwa kwenye mafuta moja kwa moja itaakua sio fair kwa mtu wa usafiri binafsi, ulipe Kodi ya mapato na huingizi pato lolote kupitia gari haiwezekani. TRA wameweka mfumo rafiki ambao unamuwezesha mlipa Kodi kupata debit number na control number popote alipo na kulipa kodi popote hata kwa mawakala wa bank ambao wapo maeneo mbalimbali mijini.
Walipakodi wengi tunaiogopa teknolojia ndio sababu tunapanga sana foleni.
pia walipakodi wengi tunasubiri deadline ndipo tukalipe kodi na kufanya foleni kuwa kubwa, hutosikia mtu analalamika foleni mwezi wa saba, wa nane, wa kumi na kumi na moja, ila ni tar 25-30 za miezi ya mwisho wa kipindi cha kulipa kodi. Kwaio sioni hilo kama ni tatizo upande wa mamlaka.
 
Back
Top Bottom