EMMANUEL JASIRI
Senior Member
- Feb 2, 2015
- 150
- 84
Mimi ni mjasiliamali mdogo mdogo,nayajua maumivu tunayo yapitia sisi wajasilia mali wadogo.Natambua uwepo wa wafanya biashara weye mitaji mikubwa ambao wamejigeuza kuwa machinga kwa lengo la kukwepa ulipaji kodi.
Hata hivyo wapo wengi ambo ni machinga halisi,pia wapo pia ambao hapo awali walikuwa na mitaji mikubwa lakini kwa sasa wamefilisika na kuamua kuchukua vitambulisho vya umachinga na kisha kuanza kudunduliza upya.
Nimesoma tangazo la TRA linalo sema,hatapewa kitambulisho cha umachinga mtu ambaye amekuwa na TIN Number,sasa kama mtu ameshuka mtaji toka milioni kadhaa na kuwa na mtaji wa elfu ishirini tu,japokuwa hapo awali amewahi miliki TIN na sasa kashuka,nasi tunajua maisha yana changamoto nyingi huyu anawekwa wapi?
Pia tangazo la vigezo vya kupata kitambulisho cha machinga linasema kuwa,machinga ni yule ambaye mauzo yake hayazidi 11,000 TTRA mauzo kwa kawaida yanaweza kushuka sana au kupanda sana,kuna siku ambapo inakuwa kama ni siku ya bahati kwa machinga maana anaweza akatokea mtu mmoja t akafanya manunuzi makubwa hata ya elfu hamsini,nanyi mnasema kigezo ni tshs 11,000 tu,je hamuoni mna watengeneza wajasilia mali mazingira ya kuwadanganya na kuanza kukimbizana.
Naamini nyie TRA mpo ofisini tunao itambua hali ya huku ni sisi,hivyo msiweke kanuni na sheria kwa mitazamo yenu,nacho kiona mimi kwa hivyo vigezo hamtusaidii ila mna tukwamisha.
Sasa niambie kuwa mnataka mauzo yawe 11000 tu,na je mmefikiria katika faida yake ni kiasi gani,maana hapo kuna mtaji na faida ,na bado,hivi kumtakia mtu kuuza tsh 11000 tu ili umpe kitambulisho mna maanisha nini,maana hicho ni kipato kidogo sana mnacho mkadiria mtu apate,ina maana akijiongeza akapata zaidi maana yake mnataka kumbana,hivi kweli ungekuwa ni wewe afisa ungeweza kumudu gharama za maisha kwa mauzo ya 11000 kwa siku?
Ushauri wangu mauzo tsh laki moja kushuka chini mngewatambua kama machinga,naamini katika laki moja kwa uzoefu wangu faida ni elfu kumi mpaka elfu ishirini,mtu wa kipato hicho bado yupo chini sana kiuchumi.
Mtu anaye uza tsh 11000 kwa siku ni mtu ambaye yuko hoi ,ana hitaji kusamehewa tu,maana hata mlo kwa siku inawezekana ni mmoja tu.
Kwa uzoefu wangu mtu anaye uza tshs 11000 kwa siku,maana anapata faida ya tshs 2000 hadi 3000
TRA Mpo ofisini,ugumu wa huku mtaani sisi ndio tunao ujue,tafadhali angalieni kwa makini taratibu zenu,vinginevyo mna tuumiza.