BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imesema moja ya Wajibu wake ni kuendelea kuhamasisha ikiwemo kutoa Elimu ya Mlipakodi kwa Watanzania ili watambue thamani na Umuhimu wa Kufanya hivyo ikiwa ni kwa Maendeleo yao na Maslahi mapana kwa Taifa.
Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam leo Agosti 30, 2024 na Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka hiyo John Walalaze wakati wa Mkutano na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.
Amesema Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa Maendeleo ambayo yanaonekana kwenye Sekta Mbalimbali, ni matokeo Chanya ya Ukusanyaji wa Kodi kutoka kwenye vyanzo kadhaa ikiwemo kundi la Wafanyabiashara nchini.
"Kuna vitu viwili hapa duniani ambayo haviepukiki, cha kwanza ni Kifo na kingine ni Kodi, kwa hiyo kama tunaendelea kuwa hai ni lazima tuhakikishe tunalipa kodi kwa mustakabali wa maisha yetu na vizazi vijavyo" amesema Walalaze.
Awali Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile akizungumza wakati wa Kikao hicho, ameeleza kwamba ni Muhimu Elimu ya Kodi ikaendelea kutolewa kwa Wananchi, huku akisisitiza Serikali iwe na Utamaduni wa kutoa Mrejesho kwa Wananchi Juu ya Namna Kodi hiyo Ilivyotumika kwenye maendeleo.
David Rwenyagira ambae ni Mhariri mkuu wa Wasafi Media, akizungumza kwenye mkutano huo, ameshauri kuwe na njia nyingine mbadala na Rahisi kuweza kubaini Bidhaa bandia ili kuendelea kudhibiti mianya ya Ukwepaji kodi kwa Makusudi.