Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Mazda CX-7 2.3 DISI MZR 5 Door
Gari hii ni ya mwaka 2007 na inakaribia kufika miaka 10
Nimejikakamua kununua gari hii kwa pauni za Uingereza 3,700 kupitia Auto Trader.
Kuhusu gari hii:
Ni right hand Drive
Ni SUV
Ukubwa wa Engine ni 2261cc
Ni 4x4
Speed yake ni 130
Imetembea Kilomita 62,000
Ni manual gear na inatumia 2.3 L ikiwa ni mafuta ya Petroli.
Sasa kwa mujibu wa kikokotoa cha TRA kwenye tovuti yao, hakuna maingizo ya gari kama hili isipokuwa kama lingekuwa limetokea Japan
Ila wanachosema ni kwa mimi kujaza anuani yangu ya barua pepe , namba ya simu na details za gari halafu watanijulisha gharama halisi.
Mwishoni wanasema katika ujumbe wao kama inavyoonyesha hapo chini:
STEP 8
After completing the vehicle details submit the details for TRA to include the missing model on the next release by clicking: Send Details
STEP 9
After sending details, the following message will appear.
Na hapo chini wanatoa msisitizo wa hii ya kutuma taarifa za gari kwa wino mwekundu kwamba:
The vehicle details have been sent to TRA technical team and your request will be accommodated in the next release of this calculator. You may proceed with your declaration in the normal procedure
Kwanini wasiweke wazi kila timu kwenye kikokotoa hicho badala ya mimi kuwapigia simu ili wanipe hesabu kamili kuhusu ushuru watakaonitoza?
Je hio ni hatua sahihi ya kufanya kwa TRA?
Kwanini kikokotoa hakikidhi mahitaji ya wateja wote yaani wale wa Ulaya na wale wa nchi kama Japan?
Mbona hii inaonyesha kuwepo dalili za uwizi wa pesa za watu?
Naomba ufafanuzi kutoka TRA tafadhali.