Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 614
Kuna taarifa kwamba TRA Uwanja wa Ndege wa Mwanza Idara ya Ushuru wa Forodha, wamezuia makasha kadhaa ya kampuni ya Barick Gold, yaliyokuwa yakipelekwa North Mara, kule Tarime.
Habari zinaeleza kwamba awali polisi walibishana na TRA wakitaka mizigo hiyo iruhusiwe ipite lakini baada ya maofisa wa TRA kuwa wakali na kusema sheria inataka mizigo ya milipuko kuelezwa wazi katika nyaraka ni milipuko ya aina gani na badala yake mizigo ya Barick iliandikwa "Ammunition" tu bila kusema ni baruti, mabomu au kitu gani. Ka nzi ketu kalikoruka ruka juu ya eneo la uwanja kalielezwa na Ofisa Mmoja wa Polisi Mstaafu aliyekuwapo eneo la tukio kwamba makasha hayo yalikuwa na mabomu ya kutupa kwa mkono na mabomu ya machozi.
Hofu iliyokuwapo sasa ni kwamba kutokana na matukio ya hivi karibuni ya huko Tarime na hasa baada ya kuikataa CCM, upo uwezekano mkubwa wa kwamba Barick pamoja na kuongezewa ulinzi wa polisi, sasa wanaongeza na silaha.
Upo uwezekano kwamba silaha hizo ni za kwao wenyewe wakitumia walinzi wao wakiwamo wale wanaowajiri kutoka nje ya nchi wakiwamo wale kutoka Napal wajulikanao kama GURKAS.
Lakini pia inawezekana silaha hizo zikawa ni mali ya Jeshi la Polisi ambalo kwa kawaida huwa na mikataba na Barick ya ulinzi mikataba ambayo kampuni hulazimika kulipa KIHALALI pale Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na hivyo upo wasiwasi kwamba sasa wamekubaliana hata kugharamia vifaa kwa polisi ikiwamo vile vya kukabiliana na fujo.
Kwa mwenye maelezo ya kina anaweza kutuhabarisha wakati ka-nzi ketu kanarukie pale Uwanja wa Ndege wa Mwanza kujua kama polisi na TRA wameshaelewana ama kuzibwa midomo ama la.
Miaka ya 1997 hadi mwaka 2000 wakati Bulyanhulu palipokuwa na vurugu na matukio ya ujambazi katika mgodi wa Kahama, Barick waliagiza silaha aina ya AK 47 na waliomba kibali Wizara ya Mambo ya Ndani. Bahati mbaya sana habari hiyo ikaandikwa na gazeti la RAI wakati huo chini ya Jenerali Ulimwengu na ndipo serikali ikawanyima kibali cha kuingiza AK 47 ambazo zilikuwa zitumiwe na GURKAS ambao walikuwa tayari wako Kahama.

SWALI: Je, sheria za nchi yetu zinaruhusu kampuni binafsi kuingiza silaha kali kama kweli itakuwa ni mabomu?
je, Kama serikali ilijadili na kukubaliana na suala hilo ndani ya vikao, kwanini siri hiyo isitolewe hadharani kama ile ya Mengi na Masha?