we fanya online itkuwa simple,hata ivo sina uhakika kama usemayo yanawezekana, ila turudi hapa , ukiseema provisional tax napata picha kuwa TRA wamegundua kuwa tayari ulikuwa unafanya biashara sasa hapa unataka kukwepa kodi kwa biashara uliyoishafanya, otherwise ueleze ukweli kwanza ndo upate jibu sahii. Nlishawahi usema hapa kuwa Jf na akili a watu ni kama google, ukibdili swali na majibu yatabadilika, sasa kama waataka ushauri ebu weka maelezo sahii ili michango yetu iendane na ukweli wa tatizoo lao.
Nenda kwenye website ya TRA Tanzania Revenue Authority - Home, angalia upande wa kulia kuna ONLINE services. Jaza form online. Nadhani hapa utapata jibu stahiki.
Wakuu poleni kwa majukumu. Jana nilipata kigugumizi cha mwaka pale ambapo katika harakati za kufungua kampuni yangu niliambiwa siwezi kupata TIN hadi nilipe provisional tax.
Nilimuuliza huyo afisa wa TRA inakuwaje mbona hata leseni ya biashara sijapata? Akniambia eti huo ndio i utaratibu na akanikadiria mahela kibao ambayo sijui nitoe wapi.
Jamani hivi ni kweli unadaiwa kodi kabla hujafungua hata biashara yenyewe au inakuwaje hii? TIN si bure au mimi ndio sielewi kitu hapa?
Tafadhali naombwa nieleweshwe maana wamenifrustrate moja kwa moja.