TRA wanatuumiza wafanya biashara

TRA wanatuumiza wafanya biashara

nrashu

Senior Member
Joined
Oct 4, 2010
Posts
144
Reaction score
63
Wadau,
Naomba kuanza kwa kupongeza mfumo mpya wa ulipiaji ushuru kupitia mfumo wa money transfer. Mfumo huu utapunguza kwa kiasi kikubwa upotevu wa mapato na utawezesha au unategemewa kuwezesha kupunguza msongamano na kuongeza ufanisi.

Kinachonisikitisha ni kuonekana kushindwa kwa huo mfumo kufanya kazi kwa haraka hivyo kutumika kufaidisha bandari na wamiliki wa ICD kwa kuongeza storage charges

Tunaomba kujulishwa huo mfumo umebuniwa kuongeza ufanisi au kuongeza gharama kwa wafanya biashara? Ni kwa nini pesa ifike BOT lakini ukienda TRA wanakujibu haionekani kwenye system?

Je sio kwamba kuna wakataa maendeleo wachache wanapinga mfumo hivyo wanataka kuukwamisha? Na kama mfumo una matatizo ya kiutekelezaji ni kwa nini TRA/serikali isitoe maelezo ya kina kuweka mambo sawa?

Je hizo gharama za ziada (storage) baada ya malipo nani atawajibika kuzibeba.

Tunaomba mtusaidie kwa kuwa mnatukwamisha wajasiriamali wenye mitaji midogo.
 
Back
Top Bottom