TRA wanautaratibu gani wa kutoa leseni katika kampuni ya uwakala wa Forodha (Clearing and Forwarding Co)?

mitindo huru

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2016
Posts
1,610
Reaction score
1,601
Habari za majukumu wadau,

Hivi TRA wanautaratibu gani wa kumpa mtu leseni ya kufanyia kazi za Clearing and Forwarding.

Maana kuna rafiki yangu alishafanya baadhi ya hatua kama kufungua kampuni yake BRELA, alishasajiliwa na hadi kuorodheshwa katika gazeti la Serikali na TRA, lakini hadi sasa bado hajapatiwa leseni ya kuendeshea biashara.

Wataalamu wa haya mambo nahitaji msaada wenu katika hili, maana wanasema kuna mtihani ambao inatakiwa afanye lakini hadi sasa hajui huo mtihani utafanyika lini.

Msaada wa mawazo unahitajika
 
Kampuni ya Uwakala wa Forodha ili ipate leseni ya kufanya kazi nchini Tanzania ni lazima ifanye mtihani wa Uwakala wa Forodha Tanzania unaotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kitengo cha Ushuru na Forodha ( Custom and Excise). Tarehe ya mtihani itatangazwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania, kwa watu na makampuni yote yaliyopatiwa usajili wa awali, baada ya kufaulu mtihani wa Uwakala wa Forodha, kampuni husika itapatiwa leseni ya uwakala wa forodha, ila Kabla ya kupatiwa Leseni ya uwakala wa forodha kampuni zote zinatakiwa kuwa na mtaji (Capital) isiyopungua milion 50 /= na pia kuwa na Banki guarantee isiyopungua milioni 100 /=. hivyo vyote ni muhimu hasa kwa mizigo ya Transit inayotakiwa kuwa na Bond ili kuzuia upotevu wa mizigo kunakoweza kusababishwa na wakala wa forodha husika.
Pia kuna vitu vingine ambavyo muombaji wa leseni ya uwakala wa forodha atatakiwa kuwa navyo kama Cheti kutoka Sumatra, Barua ya uthibitisho wa usajili kutoka Brela, wafanyakazi kusajiliwa mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Kuwa na Ofisi inayotambulika na mamlaka husika.
Hayo ndio mambo ya Msingi ya kuzingatia
 
Asante sana ndugu BusinessTZ kwa maelezo mazuri nafikiri yatakuwa msaada mkubwa sana kwa jamaa yangu. ila niliomba nijue mtihani unachukua mda gani hadi kutangazwa na tutajua namna gani kujua tarehe ya mtihani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…