TRA yabambikia makampuni kesi za Uhujumu uchumi, kupitia risiti zenye makosa miaka 10 na zaidi iliyopita

TRA yabambikia makampuni kesi za Uhujumu uchumi, kupitia risiti zenye makosa miaka 10 na zaidi iliyopita

mirindimo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
901
Reaction score
1,742
Wakati dunia nzima iko locked down ikihaha kupambana na Corona virus TRA wao wanahaha kukusanya kodi wavunje rekodi, nimeshuhudia kampuni zikiandikiwa barua kua mwaka 2010, 2014, 2015 zilipeleka return zenye risiti ambazo mashine zake VAT haitambuliki, hapa nilijiuliza maswali ya msingi;

1. Je anayetoa hizi mashine kwa mfanya biashara ni mtu binafsi au ni TRA?
2. Je anaetakiwa kuhakikisha kua mashine inatoa risiti halali na imesahiriwa kihalali na taarifa za mashine zinatambulika ni TRA au ni mfanya biashara?
3. Kwa nini makampuni yapigwe faini kubwa na kutishiwa kesi za uhujumu uchumi wakati makampuni yanayohusika na usajili wa hizi mashine za efd na wafanya kazi wengine walio husika kwa namna moja au nyingine wapo mtaani hawachukuliwi hatua yoyote?
4. Ni kweli serikali inafanya hivi ili ipate pesa ya kuendeshea uchaguzi na kufany kampeni??

Hapa kuna biashara nyingi zitafungwa na kuna watu wataonewa na kulazimishwa kulipa pesa ambazo kimsingi wao hawahusiki kuzilipa na wala hawakula hizo pesa. Serikali iangalie namna nyingine ya kupata pesa ya kufanya mambo yake kuliko hili la kuonea na kutesa raia wake
 
Bwashee TRA inahusiana vp na corona? Kama ulifanya mavirigiza ukashitukiwa sio kosa la tra walipe kodi yao uliyokwepa mambo yaishe hii ipo hata ulaya na amerika una kwepa kodi inapita hata miaka 20 wakigundua unalipa so is no new here
 
Mkuu hao wamefanyiwa examination/audit kutokana na return wanazosubmit. Hta kma ulievade tax ya 1990 ikibainiwa utalipa tu. LIPA KODI HALAL YA SERIKALI. Kuhusu mashine za EFD Kuna supplier ambao wako registered na TRA ndo wanaziuza. Just short ila khs kodi hta ya 1960 huko ukijulikana utalipa
 
Back
Top Bottom