TRA yavifutia riba vyombo vya moto ambavyo havijasajiliwa

TRA yavifutia riba vyombo vya moto ambavyo havijasajiliwa

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Mamlaka ya Mapato (TRA) imefuta adhabu na riba kwa vyombo vyote vya moto vilivyoingizwa nchini bila kufuata taratibu za forodha, huku wamiliki wakitakiwa kusajili rasmi vyombo vyao hadi kufikia Juni 30, 2022.

TRA imesema lengo la hatua hiyo ni kujenga ushirikiano na uhusiano mwema kati yao na walipa kodi sanjari na kuwapa motisha ya kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati pamoja na kuweka kumbukumbu au taarifa sahihi za umiliki wa vyombo hivyo.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Aprili 25 jijini hapa, Mkurugenzi wa Huduma na elimu kwa mlipa kodi wa TRA Richard Kayombo amesema msamaha huo umetolewa kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa kodi inayompa mamlaka Kamishina Mkuu kusamehe riba na adhabu.

MAGARI.jpg
 
Mamlaka ya mapato Tanzania leo naona wamekuja na habari ya kusamehe magari yaliyokuwa yanaenda nje ya nchi lakini yakawa yamezidi muda wa kukaa nchini na wale ambao walitumia msamaha wa kodi kinyume cha sheria au kubadili umiliki bila fata tarataibu.

Maelezo ni mengi ngoja niweke nyaraka yao traeli
MAGARI.jpg
 
Back
Top Bottom