TRA Tanzania
Senior Member
- Jul 16, 2022
- 128
- 370
#Dar es Salaam
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Mwenda na Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT) Bw. Emmanuel Tutuba leo tarehe 17/10/2024 wamekutana na Watendaji Wakuu wa Mabenki na Taasisi za Fedha nchini kujadili suala la Hati ya Uwakala katika ulipaji kodi (Agency Notice). Kamishna Mkuu Mwenda amesema kuwa, Hati za Uwakala ni njia ya mwisho kabisa ya kukusanya kodi na TRA itaendelea kutoa elimu na kujenga mahusiano ya karibu zaidi na walipakodi ili waweze kulipa kodi zao kwa wakati kwa lengo la kuondokana na matumizi ya Hati hizo za Uwakala katika ulipaji kodi.