kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,677
Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mbeya, imesema shule za binafsi, vyuo vikuu vya binafsi na taasisi yoyote isiyokuwa ya kiserikali zinapaswa kulipa kodi kama sheria inavyo sema.
Kauli hiyo ilitolewa na Meneja wa TRA Mkoa wa Mbeya, Arnold Maimu kwenye mkutano wa Shirikisho la Mameneja na Wamiliki wa Shule na Vyuo visivyo vya Serikali (Tamongsco).
Alisema suala la kulipa kodi kwa taasisi yoyote ile ambayo haipati msaada kutoka serikalini pamoja na vyuo vya binafsi na shule za binafsi linatokana na sheria ya mabadiliko ya sheria ya Vyuo vya Ufundi (Veta) iliyofanyiwa marekebisho na Bunge Juni, 2013.
Alisema kutokana na mabadilko hayo ni wajibu wa kila mmiliki wa shule, vyuo, taasisi yoyote isiyo ya kiserikali kuhakikisha analipa kodi hiyo ili kuipatia serikali mapato na ambazo hazitahusika ni zile zinazo milikiwa na serikali.
Kwa upande wake, mtoa mada Michael Nsobi ambaye ni Mkaguzi wa Kodi Mkoani Mbeya alisema taasisi yoyote ambayo ina waajiriwa wanne na kuendelea inatakiwa ilipe asilimia 30 mapato yake isipo kuwa inayo tegemea msaada kutoka serikalini.
Alisema kumekuwapo na changamoto ya kubadikisha fikra na mtazamo wa wamiliki ambao awali walikuwa hawalipi kodi ili wafuate utaratibu uliowekwa kutokana na mabadiliko ya sheria ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
CHANZO: NIPASHE