TradeMark East Africa (TMEA), Yafanyia Makubwa Tanzania Kupitia TWCC, Yadhamini Wafanyabiashara Wanawake Zaidi ya 200 Kushiriki Maonyesho ya 77

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Kwanza angalia, kisha ndio tuzungumze

Hii taasisi ya TradeMark East Africa, (TMEA), ambayo siku zote imekuwa ikifanya mambo makubwa kimya kimya, imeendelea kufanya makubwa nchini kwetu Tanzania. Safari hii kupitia Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania, wamewachukua wanawake wafanya biashara zaidi ya 200, wakawapiga semina elekezi ya jinsi ya kufanya biashara, wakawapaisha mpaka nchini China, kwenda kuwaonyesha wanawake wenzao wa Kichina wanafanya nini, kisha wakawarudisha nchini, wakawapa mafunzo ya kutengeneza bidhaa bora, wakawapatia nembo za ubora za TBS na Barcode, na kuwapa mitaji ya kuanzisha biashara, kisha wakati wa maonyesho ya Saba Saba, wakawadhamini kuonyesha bidhaa zao, ambazo sasa zina ubora wa kimataifa, na hawakuishia hapo, sasa wanawasaidia kuzitangaza bidhaa hizo, na kuzitafutia masoko ya kitaifa na kimataifa. Watanzania sijui tupewe nini?.

Soma na kushuhudia mambo ya TIMEA kupitia TWCC



Mungu Awabariki Sana Hawa Jamaa
 
Je hao akina mama ni daraja gani ni hawa wa chini au wazito? Maana bongo fursa kama hizi unazisikia baada na siyo kabla.
Wanawake wafanyabiashara wadogo wanaofanya ujasiriamali wa kuzalisha bidhaa ndogo ndogo za matumizi ya kawaida, huko China, kiwanda ni just a backyard. Mfano huwezi amini, Tanzania mpaka hapa ninapoandika, hatuzalishi toothpick, tuna import kutoka China!.
P
 
Je hao akina mama ni daraja gani ni hawa wa chini au wazito? Maana bongo fursa kama hizi unazisikia baada na siyo kabla.
Na yawezekana ndivyo ilivyo kuwa, watu wameweka ndugu zao tunakuja kusikia baada yaishi kuisha.
 
Kiukweli kabisa, huyu mtu aliyeifanya kazi hii, akitokea kuja kuchaguliwa kuwa Mwakilishi wa Tanzania ndani ya EALA, you can just imagine atafanya nini!. Kama amaweza kufanya yote haya akiwa just a journalist, akitokea akawa mbumbe wa kitu kama EALA, si Tanzania itapaa?. Au mnasemaje wanabodi?.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…