SoC04 Traffic against time management

Tanzania Tuitakayo competition threads

Princebaric

Member
Joined
Oct 29, 2021
Posts
5
Reaction score
1
Hi my fellow Tanzanians, wengi wetu tuna ndoto ya kuweza kuiona na kuifikia Tanzania tuitakayo lakini hatujaweza kuifikia kwa sababu ya changamoto mbalimbali. Binafsi nmeangalia hili suala la usafir wa barabarani na changamoto zake.

Sidhani kama kuna mtu ambaye hatumii barabara na anaishi kwenye moyo wa Tanzania ambao ni Dar es salaam.

Hili suala la traffic limekua kichocheo cha kuzolota kwa baadhi ya shughuli ndani na nje ya Dar es Salaam kwa maana linamuathiri kila mtumiaji wa barabara kuanzia kwa mwanafunzi adi HR wa kampuni kubwa.

Nkizungumzia kwa uchache baadhi ya athari ambazo zitokanazo na msongamano barabarani ni kama, wanafunzi hufika mashuleni kwa kuchelewa na wakiwa wamechoka tiyari jambo ambalo huathiri elimu yao pia na saikologia yao katika ukuaji.

wapo wagojwa wanaopata shida kwenye foleni ya magari pamoja na wauguzi wa hospitali mbalimbali bila kusahau kuwa wapo walioshidwa kufikia ndoto zoa sababu walichelewa kwenye usahili.

Hili suala la foleni ndani ya jiji la Dar es salaam bila kulipatia ufumbuzi tunaweza kuchelewa sana kuiona Tanzania tuitakayo.

Mapendekezo yangu hapa ninatamani kuwepo na revolution flani ndani ya sekta ya traffic police.

Binafsi naona barabara ziko sawa lakin msongamano unachangiwa na askari wa usalama barabarani wanaosimama kuongoza magari japokuwa kulishawekwa taa kwa ajili ya kuongoza magari.

Natamani zifungwe computerized camera system kwa ajili ya kuongoza magari na wapunguzwe askari usalama barabarani maana watakuwa wanaweza kufatilia matukio ya usalama barabarani katika computer na baadhi wawekwe kwenye maeneo yasiyokuwa na changamoto ya msongamano kwa ajili ya ukaguzi wa leseni pamoja na makosa mengine ya madereva .

Pia kuwepo msako wa kubaini na kuondoa kabsa (DMC) Yaani vehicle on dangerous mechanical conditions ambazo pia huchangia katika kuzolotesha shughuli nzima ya usafiri pamoja na usalama Kuwepo na nidhamu kwa hao Askari usalama watakaobaki barabarani hili kusaidia kupunguza kabisa ucheleweshwaji.

Time is money na ni matumaini yangu kuwa suala la time management likizingatiwa linaweza kuwa chanzo cha ujenzi wa Tanzania tuitakayo maana Tanzania tuitakayo si bidhaa kwamba tunaenda turkey tunainunua na kuileta No, bali ni kupunguza kama si kuondoa changamoto ambazo zinaizuia Tanzania katika ukuaji.

Jitihada kali na bidii vyapaswa kuzingatiwa katika kuijenga Tanzania tuitakayo na suala la nidhamu ya barabara na kupunguzwa kwa foleni ambayo uchewesha zaidi ya asilimia 70 ya shughuli za kila secta natumai tutaweza kuisogelea Tanzania tuitakayo.
 
Upvote 4
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…