Ni kweli kabisa Arusha1 anavyosema, huu utaratibu ni tofauti na wengi wanavyoufahamu.
Kuna utaratibu wa kawaida kama tulivyozoea wengi na watanzania kwa ujumla rushwa ni k2 cha kawaida. Utaratibu huu wa kawaida ni kwamba RTO(Regional Traffic Officer) anakuwa analetewa fungu kwa kila traffic kutegemea na kitengo, kifaa, sehemu aliyopangiwa.
Mfano:
Ukipdwa tochi, ile inayosoma speed ya gari kuna hela lazima ulete jwa RTO jioni wakati wa kufunga kazi hii haihusiani na ofisi halafu ulete ya ofisi kisha ubakiwe na ya kwako wewe traffic police.
Hivyo hivyo atakayepewa pikipiki, gari ya kukimbiza magendo n.k. na utapeleka hela siyo tu kwa RTO, hata kwa RPC, na wengine walio chini ya hao kutegemea uko kitengo gani.
Sasa huu ni utaratibu wa kawaida ktk nchi hii.
Utaratibu mpya wa kitengo cha traffic police pale Arusha ni tofauti/mpya.
Huu utaratibu naweza kuuhusisha na either chama au serikali.
UPO HIVI:
Traffic police anatakiwa apeleke polisi magari 10 yenye makosa kwa mwezi(haijalishi kosa hata kubambikizwa kama ukionekana uko kamili ktk gari lako) ili upigwe faini ya 30,000Tshs.
Wengine wanasema wanatakiwa wapeleke gari 20 per day.
TATIZO:
Trafic police wamekuja kusababisha usumbufu wa hali ya juu ktk mji wa Arusha. Kwa wale wanaoufahamu mji wa arusha(Arusha town) trafic police ni wengi na wanasimamisha gari kila kituo kama unataka kuwahi ofisini/hospital/kuswali au popote ina maana labda upite usiku.
Kona ya technical wanakusimamisha uwe unaenda ngarenaro au umetoka/sakina mianzini wapo, sanawari b4 mataa wanakusimamisha, baada ya mataa wanakusimamisha, philips wanakusimamisha, ngulelo hawa, kwa mrefu hawa, nduruma unapigwa mkono.
Kutoka kituo mpaka kituo haizidi 1.5km ingawa vituo vingi ni less than 1km.
Vituo vyote lazima wakusimamishe ukifanikiwa kupita bila kusimamishwa ni kwamba wako busy kwenye magari waliyoyasimamisha.
Wanamuuliza dereva kila kitu kinachotakiwa kuulizwa, akiona umekamilika anakuchomekea lolote 'wewe nakusimamisha husimami unakimbia' twende kituoni. Anakupeleka.
MAPATO:
Inasemekana kitengo cha trafic police wanakusanya kiasi cha 6-7million per day kwa hapa Arusha mjini.
Cha kujiuliza: huu utaratibu si wa kawaida na je nani kawatuma, hizo hela wanapeleka wapi?