Traffic Queue na uchumi

Traffic Queue na uchumi

Paschal Matubi

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2008
Posts
235
Reaction score
303
Wana JF. Ni wapi tunaweza kupata statistics zinazoonyesha ni uchumi kiasi gani unapotea kwa kusababisha na msongamano wa magari au traffic jam.
Unatoka nyumbani saa 12:00 unafika kazini saa 2:30 na wakati mwingine. Ni kama vile muda wa kazi rasmi unaanza saa 03:00. Jamaa wa Mlimani City sijui kama wao ndivyo walivyowaza. Wao wanafungua ofisi saa 04:00 na hawana haja ya kujidanganya kfufungua saa 02:00 kama ulivyo muda wa ofisi zingine.

Sasa kama kweli muda wa kuanza kazi ni saa 02:00 na mtu anacheleweshwa hadi saa 03:00 ni vijisenti vingapi vinapotea kwa huo kuda uliopotezwa? Hiyo ni mmoja tu. TUnaona foleni zilivyo na speed ya kinyonga anayesindikiza harusi. Je msululu wote ule uliochelewa kazini umepoteza mamilioni mangapi?

Hiyo ni kwenda kazini. Uje sasa shughuli za kazi. Uko kazini unatoka Posta kuwahi ndege JNIA. Foleni lazima iwe kichwani mwako.

Njoo sasa jioni wakati wa kurudi nyumbani. Safari ya kilomita kumi inatumia masaa mawili tena kwenye lami, na hapo haijanyesha mvua

Kama humu JF kuna wanauchumi watusaidie tujue kiasi kamili kinachopotea. Huenda kinachopotea ikagundulika ni ufisadi ambao haujawahi kufikiriwa.
 
Back
Top Bottom