Kuna utaratibu unafanywa na Jeshi la Polisi siku za hivi karibuni kwa kulazimisha Daladala hasa zinazoelekea Mbezi ya Chini, Makumbusho, Kawe, Tegeta kuwa lazima ziingie Kituo cha Daladala cha Mawasiliano (Simu 2000) unakera sana.
Ukiangalia hakuna hata jambo la msingi zaidi ya kupoteza muda wa Abiria tu. Daladala zinaingia na kutoka bila kuchukua wala kushusha Abiria yeyote.
Kama Serikali inakosa mapato ya Ushuru iangalie namna nyingine sio hii ya kulazimisha Magari kupita Vituo ambavyo havina abiria wa magari hayo.
Ni utaratibu wa kawaida kabisa
Gari inayo enda Kinyerezi kutoke mnazi m1 au muimbili na kuna zile za Bonyokwa lazima iingie Segerea kwanza
Gari inayotenda Makumbusho, Kawe kutokea popote lazima iingie mawasiliano
Gari zinazo enda bunju kitokea Mbezi, Mawasiliano, Makumbusho, Kawe na Morocco zinatakiwa kuingia nyuki kwanza ndio ziende Bunju, ila hii stand ya nyuki ni ndogo na junction ya kuingia nyuki ni single way na ni ndogo kulinga na wingi wa magari na ndipo njia 4 zinapoishia
Gari zote zinazo enda gongola mboto au zinazoenda kisarawe na chanika lazima ziingie kigogo sokoni
Gari zinazoenda Mbezi au kutoka Mbezi kupitia Maramba mawili kwenda popote ni lazima ziingie Kinyerezi stand
Gari zote zinazoelekea Kibaha, Mlandizi, Chalinze na popote Tanzania mpaka mabasi ya mikoani ni lazima ziingie stand mpya ya Kibaha ndio ziendelee na safari
So hiyo ishu ya mawasiliano/Simu2000, kuepuka huo usumbufu wa kuchelewa, wewe kama abiria ndio ujitahidi kuwai ili hata ukilazimika kuingia huko usichelewe[emoji2960][emoji2960][emoji2960]