KERO Trafiki mnaoweka kijiwe Kiluvya, Kibamba, Mbezi na maeneo hayo mnalitia aibu Jeshi la Polisi

KERO Trafiki mnaoweka kijiwe Kiluvya, Kibamba, Mbezi na maeneo hayo mnalitia aibu Jeshi la Polisi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

lucas meshack

Member
Joined
Jul 21, 2015
Posts
14
Reaction score
8
MDAU

Traffick Mkoa wa Pwani mnalitia aibu Jeshi la Polisi, mnajipanga barabarani kila kituo cha daladala mnachukua buku (1,000) za madereva wa daladala.

Mnakaa kituo cha Kiluvya madukani, Bwawani, Gogoni, Kibamba shule, magari saba na kituo cha Mbezi Mwisho. Vituo vyote hivyo makondakta wanatoa buku buku.

Hata kama mliruhusiwa kuchukua pesa ya kubrashia viatu lakini siyo kwa utaratibu huo kwa sababu mnatuchelewesha sisi abiria kuwahi kazini.

Tena traffick wengine wanachukua buku hadharani, wengine wanajifanya eti wanakagua gari wakati huo kondakta anamfinyia Kwa nje hilo buku.

IGP, Wambura zungumza na vijana wako wanalipaka matope Jeshi la Polisi
 
Hao trafiki wa Pwani ni moto sana, nakumbuka siku moja nipo na brother tunatoka mwanza kwenda Dsm, the whole jounery hatujapigwa mkono na tulikua makini lakini baada ya kuvuka Moro kuingia Pwani tulishimamishwa kama mara 4 na kote ilikua wanapiga maokoto ( kifupi zaidi ya mara tatu walikua ilikua ni usumbufu na kutaka pesa)
 
Hii nchi kila mtu kwa nafasi yake anapiga dili za pesa.
Kikubwa ni wewe mwananchi kukataa kutoa pesa kizembe kwa issue za kikhanithi.
 
Hapa mwanga mkoani kilimanjaro wanaomba mpaka ndizi mbovu,marachichi ,mayai nk !! Njaa tupu
 
Barabara nyembamba ndiyo mtaji wao hao,usipofata mistari tu wanakuvamia kama kijiji utoboi.
 
Back
Top Bottom