Trafiki Shinyanga Angalieni zile Trafific Light za Phantom Pale

Trafiki Shinyanga Angalieni zile Trafific Light za Phantom Pale

luangalila

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2014
Posts
6,346
Reaction score
6,928
Eneo la Phantom sio geni kwa waenyeji wa Shinyanga na wanao pita highway kwenda au kutoka Mwanza. Hili eneo ni kero sana hasa wakat wa Jioni

Sio ajabu ukiwa pale ukaona Gari dogo lina vuta barabara ilihali Traffic light inawaka taa NYEKUNDU kuashiria kusimama

Sio Ajabu gari ukiwa pale eneo la Phantom kuona gari na vyombo vingine vya moto kama bodaboda kuvuka barabara ilihali Traffic light ikiwaruhusu watembea kwa mguu kuvuka barabara toka ng'ambo moja kwenda ng'ambo ya pili

Jeshi la Polisi hasa Kitengo cha traffic nafikir hampaswi kujisaulisha wajibu wenu, hili eneo ni kero kwa watembea kwa miguu, wazee wana vuka eneo lile tena kwa Changamoto sanaa vile vile watoto.
Nitoe rai kwa jeshi letu fikeni eneo la tukio kukamata na kupiga fine vyombo vya moto vinavyo vunja sheria za barabaran makusudi kabla ajali hazija anza kuzuka ..


Last Month jeshi la polisi mliweka nguvu kubwa kuwazuia wale vijana wanao bet mabasi kupita mapema eneo lile mlifanya kazi nzuri lkn bado hamjaimalizia kwa kuvizibiti ivi byombo vya moto vinavyo vunja sheria za barabaran .
 
Back
Top Bottom