KERO Trafiki Tabora saidieni kupunguza msongamano karibu na Stendi Kuu hasa wakati wa usiku

KERO Trafiki Tabora saidieni kupunguza msongamano karibu na Stendi Kuu hasa wakati wa usiku

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Torra Siabba

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
243
Reaction score
287
Ndugu Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani hapa Tabora, Mh Magayane sisi wakazi wa hapa tunakuomba udhibiti suala la msongamano wa magari eneo la Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo Mikoani hususan jioni maana hakuna utaratibu maalumu kila basi linashusha njia kuu jambo linalisababisha msongamano.

Ikifika Saa 2 Usiku na kuendelea, tunashuhudia Mabasi yanashusha abiria barabarani, hali hiyo inachangia msongamano kama vile kuna msafara unapishwa, kumbe wapi.

Mabasi mengi yanaziba njia na kusababisha usumbufu kwa wapita njia wa kawaida maana msongamano unakuwa mkubwa bila sababu, hivyo hii changamoto kusema ukweli itatuliwe kwa uharaka maana haijaanza leo wala kesho.

Tusaidieni maana muda huo askari wanakuwa maeneo mengine kwanini pale stendi wale waliomo ndani wasisaidie kwenye hili?

20250107_195211.jpg
20250107_195204.jpg
20250107_195206.jpg
 
Back
Top Bottom