Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
''TRAGIC COMEDY'' WAKO WATAKAOCHEKA WAKO WATAKAOLIA
Kwa umri wangu huu baada ya kula chakula cha mchana kitanda kinaniita kujipumzisha kidogo.
Lakini kama kawaida kutakuwa na hiki au kile mtu unataka uchungulie katika simu na ikibidi nifungue mtambo ikibidi kwani huko ndiko Maktaba ilipo.
Nasikia, ‘’Hodi, hodi, hodi.’’
Nafungua nawaona watu wa stesheni moja maarufu sana wako mlangoni pangu wananiambia wamekuja kunihoji kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964.
Nikawakaribisha ndani.
Si wageni hawa vijana wameshafika kwangu mara kadhaa kwa kunihoji.
Wananiambia kuwa wangependa wanihoji kuhusu sherehe za mapinduzi.
Akili yangu inajisemeza yenyewe kuhusu hili neno, ‘’sherehe.’’
Sherehe ndani ya msiba.
Mimi kwa haraka sana nikawaambia kuwa suala la mapinduzi ya Zanzibar ni historia inayotakiwa ichukuliwe kwa tahadhari kubwa sana kwani kwangu mimi na kwa wengine si suala la kuchukuliwa kwa sherehe kama wanavyotaka kunihoji.
Nikawaambia kuwa mapinduzi kwa baadhi ya watu huwakumbusha vifo vya ndugu zao siku ya mapinduzi na baada ya mapinduzi.
Historia ya mapinduzi si jambo jepesi kama wanavyolichukulia.
Wale vijana hawakutegemea maneno yale kutoka kwangu.
Nikaona sura zao zina mchanganyiko wa kushangaa na mashtuko.
Nikawaambia, ‘’Mimi baba yangu alikuwa na rafiki zake wawili, Jaha Ubwa na Abdulaziz Twala wanamapinduzi na wana ASP kindakindaki.
Hawa waliuliwa baada ya mapinduzi na baba yangu alikuwa na picha walipiga wote watatu picha hii baba alikuwa ameitundika ukutani nyumbani kwetu.
Baada ya kuuliwa hawa rafiki zake wawili picha ile aliitungua pale pengine kwa uchungu kuwa hakuweza kuitazama ile picha kwa majonzi yaliyokuwa moyoni kwake na pia pengine kwa hofu ya yeye kuogopa asije kuhusishwa na wale watu ‘’wabaya,’’ ambao kwa ubaya wao hukumu yao ilikuwa ni kuuliwa.’’
Niliwaonyesha hawa vijana kitabu cha Dr. Haritht Ghassany, ‘’Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,’’ nikawauliza kama wamepata kusoma kitabu hiki.
Hata kukiona au kukisikia ilikuwa bado.
Niliwaeleza kuwa kitabu kile kina maneno ya yale yaliyotokea Zanzibar wakati wa mapinduzi kutoka kwenye vinywa vya wahusika wenyewe na wengi wao wametangulia mbele ya haki wakiwa na majuto kwa yale ambayo mikono yao imetanguliza.
Nikawaambia wao kama waandishi wajitahidi sana kusoma.
Juu ya haya yote tulifanya kipindi kifupi kuliko kawaida cha mapinduzi lakini yale maswali ambayo naamini walikusudia kuniuliza hawakuniuliza.
Hawakuweza tena kuwa na moyo wa kuniuliza nilikuwa nimewafanulia pazia kuona upande mwingine wa jukwaa.
Picha ya kwanza ni Mohamed Omari Mkwawa, John Okello na picha ya mwisho askari wa mapinduzi akiwa katika ulinzi wakati wa mapinduzi.