joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Hii imekuja kipindi ambacho waganda wameshitushwa na habari ya China kuwanyima mkopo Kenya wa kufikisha reli ya SGR hadi Malaba. Kutokana na hali hiyo, Uganda haiwezi tena kupata mkopo wa kujenga reli ya kuunganisha na Kenya, kwahiyo njia pekee ya usafiri wa reli ya kuaminika ni kupitia Dar.
Serikali ya Tanzania sio tu inajenga reli mpya ya SGR, bali pia inakarabati reli ya zamani na kununua reli maalumu zenye uwezo wa kubeba train na kuzivusha hadi Port bell Uganda ili ziendelee na safari, pia Tanzania inanunua meli kubwa na yakisasa ya abiria itakayofanya safari zake kati ya Uganda na Tanzania ili kupunguza gharama za usafiri.