Travelholic (wanaopenda kusafiri) na adventurers tukutane hapa

Fibanochi

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2018
Posts
476
Reaction score
1,018
Habari wanajamvini, naona taratibu week end inaanza, back to the topic, naomba Leo tujuane watu tunaopenda kusafiri safiri, iwe nje au ndani ya mipaka ya nchi.

Najua kwa jamii yetu ya kitanzania ni aghalabu sana kuona mtu anasave au anatenga kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya kusafiri au kutembea sehemu fln. Lkn kadri siku zinavyoenda naona hobby hii inazidi kushika kasi miongoni mwa jamii ya kitanzania.

Wacha nikwambie kusafiri ni raha, kunaufanya ubongo upate chakula chake 'maarifa mapya, mtu anaesafiri anajifunza mmb mengi sana kuanzia kubadirisha mtazamo wa mtu juu ya mmb mblmbl ya ulimwengu, kujifunza, n.k

Je wewe mkuu ushawahi safiri wapi nje au ndani ya nchi? Kuna adventure gani huwezi isahau? Na nini ulijifunza khs hy safari yako? Ni wapi uliwahi kwenda ungetamani urudi tena na kwanini? Ni sehemu gani usingependa urudi tena?

Ni chombo gani cha usafiri unapendelea kutumia?
Mimi binafsi nimeshasafiri sehemu kadhaa hapa nchini na nje ya nchi, kila safari kwangu huwaga mpya, huwa naenjoy kila moment napokuwa safarini iwe binafsi au kikazi...kwa sehemu ambazo nimeshafika kwa hapa Tz ni moja tu so far, huwaga hainichoshi kwenda ni Mwanza. Mwanza ni mji mzr kwangu mm, watu wake wakarimu sana km alivyoimba Remmy Ongala (&%#mwanza mji mzr, mwanzaaa), ya pili ni zenji......sehemu ambayo ilikuwa changamoto kwangu ni Katavi, aisee kule kama Congo , yani umbali kama wote vile! Unakaa kwenye gari mpk unajisahau, ila kuna kuku wa kienyeji wa kutosha....kwa nje ya Tz nimetembea sy nchi nyingi sana ila, kati ya miji niliyotembea nilipapenda sana NY, aisee hili jiji lina shangwe kama zooote vile, yani hakuna kulala hasa majira ya joto May to september , jiji muda wote lina vibe, yani maduka yanakesha na watu wanafanya shughuli zao kama saa sita mchana....
20190111_165929.jpeg
20190111_165606.jpeg
20190111_165624.jpeg
 
Napenda kusafiri sana sana

Safari yangu ambayo hua haitoki akilini ni kwa mara ya kwanza napanda meli kwenda unguja nikiwa na mama

The way naiona meli kwa nje, kama jumba hivi jinsi linacheza kwenye maji ndio likanifanya nitake kubakia dar na safar iishie pale kwa kweli kwa kipindi kile kabla bakhresa hajatengeneza hata gati zile kule unguja meli ilikuwepo ya nafuu nayoijua ni flying horse nikapanda kiroho ngumu shida ikaja kuingia kwenye meli kuliwekwa kitu kama chaga za kitanda unakanyagia uingie kwa chini naona maji nikahisi kizunguzungu ikabidi waje kunibeba nikaenda kukaa upande ambao naona view ya bahari vizuri na kwa ubavuni kulikua na meli ya mv mapinduzi ndio hapo taswira za titanic zikaanza kunijia kichwani nilikosa raha mpaka nafika unguja sikulala

Baada ya hapo nikazoea kidogo safar za huko japo woga uko pale pale na always meli ikifika mkondoni lazima nijisikie hovyo hovyo

Nilienjoy sana kutembelea makumbusho ya kale nilifrah mno nilikula vingi vya baharini ambavyo vengine sikuwah kuvila kwenye maisha yangu

Safari yangu nyingine nilivyokwenda amboni caves kuanzia kwenye kile kibao amboni caves ni kama km kadhaa na kuonesha kilipo ile miti miti ukijani wake madhari na mawe yalivyojipanga mpaka ndani mle japo kunatisha nilifrahia

Safar zangu ambazo zilikua na manufaa nilivyotembelea sisal estates karibu zote za hapa tanga, kuna moja iko sakura ni mbali mana mnaacha barabara ya kipumbwi mnatokomea maporini huko hata mtandao hakuna ni airtel tu inashika

Na shamba moja lipo mnazi ni mbali sana unakaa kwenye gar alienda dar au moshi kafika kala kaoga sisi bado tuko kwenye gar kuanzia alfajiri saa kumi na moja mpaka saa tisa ndio tunaingia eneo karibu na shamba bado kulikagua shamba kuongea na sisal estate's manager bado hamjakagua korona nilifika home saa saba usiku nimechoka vibaya sana

Safari yangu nyingine nakumbuka nilikwenda tarangire national park nilienjoy si haba
 
Napenda Moment ya kusafiri sana " huwa inanifariji na kunifanya nisahau shida zote ... haswaa napokuwa kwenye chombo cha usafiri " huku nikiwa natizama mandhari ya sehemu mbali mbali ambazo chombo hicho huwa kina pita ...

Kwakweli kusafiri ni jambo " lenye afya " kwa ubongo ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana, me pia nimepanda boti mara kadhaa kwenda Unguja, nachojua safari za majini hasa baharini huwa hazitabiriki, yani kuna siku bahari inatulia unafika ukiwa fresh, na kuna siku utajuta kuzaliwa ha ha ha...Ila safari yangu ya kiadventure ilikuwa toka Dar na kwenda Mpanda na kurudi Dar ndani ya 24 hours, aiseee siwezi sahau hii, niliumwa mgongo na kiuno miezi kadhaa.
 
Naam, umenena vyema, bila shaka utakuwa unapenda kukaa siti ya dirishani wewe...ha ha ha!
 
Safari yangu ambayo sitaisahau nilitembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire,asee ile kitu ni safi sana,huduma za tour guides ni nzuri sana,pia katika mzunguko wote nikamalizia na lodge yao inatwa Sopa (Sopa lodge),ile kitu ni hatari sana,iko katikakati ya mbuga,lakini huduma zote zipo.Sikuweza kuamini kuwepo kitu kizuri kama kile.Ni kweli unaposafiri ubongo unaachia kiasi flani hasa ukizingatia ulimwengu tunaoishi una changamoto nyingi sana na haziishi,sasa usipotoka na kukaa mbali na hayo maeneo,kwakweli unaweza kuona maisha yamesimama...
 
Hahaaa ndio mkuu ..umepatia .. huwa nikikaa na kutazama mandhari ya nje ... naanza kupata hisia fulani hivi ubongo unaweza kuanza kuniletea picture za matukio ya utotoni haswa yale mazuri... pia huwa Ubongo unaniletea picture mbali mbali za jinsi nitakavyo kuwa naishi baada ya kufanikiwa baadhi ya malengo yangu kadhaa wa kadhaa .. yenaweza kuwa malengo ya kiuchumi" kimahusiano .etc

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safari yangu ambayo sitaisahau nilitembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire,asee ile kitu ni safi sana,huduma za tour guides ni nzuri sana,pia katika mzunguko wote nikamalizia na lodge yao inatwa Sopa (Sopa lodge),ile kitu ni hatari sana,iko katikakati ya mbuga,lakini huduma zote zipo.Sikuweza kuamini kuwepo kitu kizuri kama kile.Ni kweli unaposafiri ubongo unaachia kiasi flani hasa ukizingatia ulimwengu tunaoishi una changamoto nyingi sana na haziishi,sasa usipotoka na kukaa mbali na hayo maeneo,kwakweli unaweza kuona maisha yamesimama...
Mkuu kusafiri ni tiba kubwa sana, hasa ya ubongo, kwenda mazingira ya tofauti na ulipozoea siyo tu huondoa au kupunguza 'stress' bali hukufanya uonekane mpya kabisa, ndiyo mana wenzetu walioebdelea hasa nchi za magharibi na hata mashariki ya mbali kusafiri ni sehemu ya maisha yao, na wanakuaga kbs na budget mahsusi kwa issue hiyo...Ila SOPA ni pazuri sana, patulivu, kuna lodge nyingine inaitwa Tarangire safari lodge, ina view nzr sana ya mto Tarangire, next time ukienda fikia hapo...
 
Hahaaa ndio mkuu ..umepatia .. huwa nikikaa na kutazama mandhari ya nje ... naanza kupata hisia fulani hivi ubongo unaweza kuanza kuniletea picture za matukio ya utotoni haswa yale mazuri... pia huwa Ubongo unaniletea picture mbali mbali za jinsi nitakavyo kuwa naishi baaxa ya kufanikiwa baadhi ya malengo yangu kadhaa wa kadhaa .. yenaweza kuwa malengo ya kiuchumi" kimahusiano .etc

Sent using Jamii Forums mobile app
Inakuwa kama unafanya tahajudi 'meditation' vile, unaangalia maisha yako kwa 'tv' ha ha ha!
 
Safi sana, me pia nimepanda boti mara kadhaa kwenda Unguja, nachojua safari za majini hasa baharini huwa hazitabiriki, yani kuna siku bahari inatulia unafika ukiwa fresh, na kuna siku utajuta kuzaliwa ha ha ha...Ila safari yangu ya kiadventure ilikuwa toka Dar na kwenda Mpanda na kurudi Dar ndani ya 24 hours, aiseee siwezi sahau hii, niliumwa mgongo na kiuno miezi kadhaa.
mimi hiyo safar ya mnazi ndio ilinichosha mnapiga story mpaka mnakaa kimya nafika home hoi kwa uchovu nilijua kuoga tu na kulala

Safari yangu ambayo sitakaa nikaisahau pia nilivyotaka tanga na jahazi mpaka unguja mkokotoni eti nione tu umbali na gharama nafuu lakini sikurudia ujinga huo mambo ya kuloa na mawimbi ya bahari yan hapana gua had mwili unasisimka nikikumbuka ile safar nilitapika vibaya sana na nikakoma kurudina huko ikabidi nizungukie dar
 
Duuh, pole sana mkuu lkn ulipata uzoefu, ilichukua muda gani toka TA mpk Unguja?
 
tuliondoka tanga usiku saa tisa mpaka saa kumi na mbili tukaanza kufika nungwi saa moja moja had saa mbili tukafika mkokoton halaf hatukufungiwa mashine jahazi lilikwenda na upepo lilifungwa tanga kama mashine ingefunga bas saa kumi na mbili tu tushatia nanga, speaking of experience yan nilipata si haba lakini huo usafiri unafaa wavuvi na wale walokwisha zoea kupiga makasia inatisha usijaribu labda ukaze roho
 
Ni vzr kupata experience katk maisha lkn hy aisee inipitie kushoto....too risky. Ila wavuvi wanaroho ngumu sana aisee!
 
Back
Top Bottom