TRC mpambane sana la sivyo mtakula hasara

TRC mpambane sana la sivyo mtakula hasara

LICHADI

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2015
Posts
4,491
Reaction score
12,560
Cha kwanza hizo Treni mzitunze haswa hasa hayo mabehewa Kitu ambacho kinaweza kumchefua mtu na kukimbilia mabasi ni uchafu wa Treni hasa zile za Kigoma mtu akifikiria anashuka kichwa kimejaa vumbi anaona asipande basi tu full AC.

Hakikisheni safari za Dodoma kwa siku zipo hata mara 5 kwa masa tofauti, siku hizi Dodoma Dar ni kama Moro na Dar tu Watu wanatoa GARI KILA baada ya saa kwenda Dom Hadi jioni na usiku GARI zipo, so mkileta zile habari za tuna safari moja tu Leo tegemeeni kula hasara.

Maana siku hizi mtu anakuja Dar anafanya kazi zake anajua muda wowote vyuma vya kugeuza Kurudi Dom vipo muda wowote Hana shida sasa mnatakiwa Treni siwe za kutosha mda wowote mtu awe na uhakika wa safari, mkileta habari za Leo hatuna Treni Mara sijui Leo tuna Treni moja tu umekula kwenu.

Hizo treni za umeme hakikisheni usafi n zitunzwe, mkiyaharibu hyo wateja watarudi wote mwenye Yutong.
 
Ushauri Ila TRC Ni Sikio La Kufa
Kama Wamwshindwa Dar ~Morogoro Wataweza Dodoma
 
Nauli wameweka ndogo Sana Kwa hadhi ya hizo train

Hiya train Kwa Tanzania ni Luxury Train bei mfano Dar Moro ingekuwa elfu 20 lakini hiyo ya elfu 13 wahuni watajaa na chooni kutakuwa kuchafu balaa

Sababu difference ya nauli ya basi na hiyo luxury train Kwa Tanzania ni ndogo mno

Sipati picha itakavyofurika watu ikianza safari Kwa hizo nauli ndogo
 
Back
Top Bottom