Ken Macharia ni Mkenya anayezunguka nchi mbalimbali duniani kutalii yuko Tanzania na akaona apande train ya mwenfo kasi toka Dar hadi Morogoro Kwa mara ya kwanza. Kitu alicholalamika cha Kwanza ni ucheleweshaji kukata Tiketi pale dirishani inachukua karibu dakika 10 kukata Tiketi moja.
Pili ukishakata Tiketi kuna kuchekiwa Tiketi kabla kuingia kwenye train kunachukua muda pia anasema yawezekana system hazijakaa vizuri.
Ushauri wangu binafsi Kwa TRC najua mna mfumo WA kukata Tiketi Kwa simu utangazeni Sana huo mfumo watu waujue wekeni matangazo mengi hata humu Jamii Forums,Vipindi vya tV mfano ITV kabla ya taaria ya habari watu waujue kukata Kwa simu wakafie huko.
Pili chapisheni vipeperushi kwa lugha tatu wagawieni watu wanapoingia kuwa waweza kata Tiketi wenyewe kwenye simu au mtandaoni Kwa debit card au credit card.
Mjue sasa mnaingia kimataifa mtalii awe anaweza kata Tiketi online hukohuko aliko kama ifanyikavyo kwenye ndege akifika Tanzania anakuwa tayari ana Tiketi.
Matangazo ya muhimu mno kuna siku mtazidiwa kukata Tiketi hadi train itaanza kuchelewa kuondoka na kuleta maudhi Kwa abiria.
Pili muweke sehemu ya Mpesa, Tigo pesa nk MTU akishapata kipeperushi ajaze pesa kwenye simu yake hapo halafu ajikatie mwenyewe ili muanze kuwazoeza ila Kwa wale wasioweza wakaribisheni counter na mueleze hivyo asione kama hawezi kuwa kikwazo.
Watu kujaa kulundikana Tu counter kizamani mno
Tatu mfumo wa kucheki Tiketi Kwa wanaoingia kwenye train uwe wa haraka kama ilivyo Airports.
Video Yake huyo Mkenya hii hapa
View: https://youtu.be/886LVKcMQn4?si=YfaplUhptnWBxTLg