Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Majira ya Asubuhi ya leo Desemba 4, 2024, iliripotiwa kuwa Treni ya Abiria ya Kisasa (SGR) iliyokuwa ikitokea Dar kuelekea Dodoma imekwama katika Stesheni ya Kilosa Mkoani Morogoro kwa kilichoelezwa kuwa ni hitilafu ya Umeme na hivyo kusababisha safari hiyo kushindwa kuendelea.
JamiiForums imezungumza na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Fredy Mwanjala ambaye anafafanua kilichotokea:
“Treni zetu zilisimama katika maeneo matatu tofati kutokana na hitilafu ya umeme katika gridi ya Taifa, hivyo mikoa inayopata umeme kutoka katika gridi ya Taifa yote haikupata umeme ikiwemo Dar es Salaam na Morogoro.
“TANESCO wameshatoa taarifa yao kuhusu changamoto hiyo, kutokana na kuwa Treni yetu ni ya umeme na tunalishwa umeme na TANESCO ndio maana ikatokea changamoto hiyo.
“Hivyo sio shida ya Treni, kichwa wala reli, shida ni kukatika kwa umeme katika Gridi ya Taifa, tayari umeme umerejea na ilipofika Saa tano na nusu Asubuhi hii safari zimeanza zote rasmi.”
Pia soma
~ Treni ya SGR kutoka Dar kwenda Dodoma yadaiwa kukwama tena baada ya Umeme kukatika Stesheni ya Kilosa
~ Shirika la Reli Tanzania (TRC) laomba radhi kutokana na kuchelewa kwa safari kulikosababishwa na changamoto zilizo nje ya uwezo wao
~ Treni ya SGR Dodoma kwenda Dar imekwama kituoni Mkata SGR station toka saa 1 jioni