Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Shirika la Reli Tanzania (TRC), linapenda kutoa pole kwa abiria waliokuwa wakisafiri kati ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma Januari 8, 2025 kufuatia usumbufu uliojitokeza kutokana na hitilafu ya kiufundi iliyotokea katika kituo cha Ihumwa Dodoma majira ya saa 5:38 usiku.
Tunajua kuwa safari zetu za kawaida kati ya Dar es Salaam na Dodoma zimeathirika, na tunatambua kuwa hii inaweza kuwa na athari kubwa kwenu.
Mafundi wetu wamepambana kurekebisha tatizo husika na kuhakikisha huduma zetu zinarejea kwenye hali ya kawaida.
Soma, Pia: Treni ya SGR ya Dar - Dodoma imesimama Morogoro kwa Saa Mbili, kisha imezima tena kabla ya kufika Dodoma
Treni zilizoathirika ni:
• Treni iliyoondoka saa 12:55 jioni siku ya Jumanne Januari 7, 2025 kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma, iliyotarajiwa kufika saa 5:01 usiku badala yake ilifika saa 7:00 usiku.
• Treni inayoondoka saa 11:15 asubuhi siku ya Jumatano Januari 8, 2025 kutoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam, iliondoka saa 3:05 asubuhi.
• Treni iliyotakiwa kuondoka saa 12:00 asubuhi tarehe 8 Januari 2025 kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma, iliondoka saa 12:30 asubuhi.
• Treni iliyotakiwa kuondoka saa 3:30 asubuhi siku ya Jumatano Januari 8, 2025 kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma, iliondoka saa 11:55 asubuhi.