TRC yawaasa Abiria kupanga safari zao mapema kuanzia kesho Kwenye Vituo vya Magufuli na Samia

TRC yawaasa Abiria kupanga safari zao mapema kuanzia kesho Kwenye Vituo vya Magufuli na Samia

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Wanajukwaa!

Jiji katika siku hizi 2 litakuwa bize sana so kila kitu kitakwenda kwa speend sana
===================
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limewaomba abiria wanaofanya safari zao kati ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma kupanga vizuri namna ya kufika mapema vituo vya stesheni wanavyotarajia kupandia treni hususani kituo cha Magufuli jijini Dar es Salaam na cha Samia jijini Dodoma.

Kutokana na taarifa iliyotolewa leo Januari 26, 2025 na shirika hilo kufika mapema kwa abiria hao itaepusha usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na baadhi ya barabara kufungwa kupisha mkutano wa kimataifa wa Nishati unaoanza kesho Jumatatu.

Awali, taarifa ya Polisi iliyotolewa jana Jumamosi Januari 25, 2025 na Kamanda Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Jumanne Mulir, imesema kutokana na ugeni wa viongozi watakaokuja kwenye mkutano huo, barabara zitafungwa kwa muda kuanzia leo.

"Katika hatua nyingine kufuatia kufungwa kwa muda barabara hizo na Jeshi la Polisi Tanzania, TRC inapenda kuuarifu umma na abiria wanaotarajia kusafiri kati ya Dar es Salaaam na Dodoma Januari 27 na 28, 2025 kuwa treni zote ikiwemo ya Express, zitasimama kupakia na kushusha abiria katika kituo cha Pugu na kwamba utaratibu huu utahusu pia abiria wa kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam," imefafanua.

Hata hivyo hatua mbalimbali zimeshachukuliwa kutokana na umuhimu wa mkutano huo ikiwemo wafanyakazi wa umma kufanyia kazi nyumbani, huku wanafunzi wa shule na vyuo kupumzika siku mbili.
 
Back
Top Bottom