Kwenye kilimo kuna ishu wanasema, 'taarifa sahihi'. Ndani ya huu msemo kuna suala la muda ambalo ndani yake tena litaamua ni muda gani sahihi wa kulima, kupanda, kuvuna hadi kupeleka bidhaa sokoni. Ukikosea hapa, una asilimia kubwa ya kupata maumivu. Trekta nyingi za kichina kwa nchini kwetu, shida ni kupata spare. Unaambiwa dunia ni kijiji utaagiza na itakufikia.
Sawa hatukatai utaagiza na itakufikia. Je itachukua muda gani kukufikia? Muda wote wakati unasubiri hiyo spare, msimu wa kulima utaendelea kukusubiri?
Je Utafaninisha na yule ambae trekta ikiharibika, akipiga simu Mwanza mjini, Morogoro, Arusha, Dodoma au Dar na akasema spare anayohitaji akataja na namba ya spare kesho jioni anaipokea na kuifunga na kazi kuendelea?
Kuna ishu ya reliability, nina uzoefu na trekta aina tatu tofauti za kichina ambazo kwa umbo, mngurumo wake na sifa zilizokua zinapewa, utasema mashine ndo hizi. Ila hakuna hata moja ambayo ililima kwa misimu miwili.
Kingine, operators wengi wa matrekta hapa Tz ni wako rough sana. Nenda huko Kibaigwa, Kiberege, Bwawani na maeneo mengine mengi ukaone jinsi swarajs, masseys, new holland na zingine nyingi zinavyoteswa. Naamini trekta ya kichina ikimaliza msimu wa kulima itakua imechakaa kupita maelezo.
Pale Nanenane Morogoro. Wale jamaa wa Suma jkt. Walileta trekta za kichina zilikaa kama miezi nje pale, wakahamishia mle ndani zika kaa karibia mwaka na hazikuuzika. Ziliondolewa kimya kimya. Nawez kukupa namba ya muhusika palepale Morogoro umuulize ni kwanini hazikuuzika atakueleza mambo mengi tu.
Mwisho wa siku wewe mteja ndo mwenye maamuzi ya mwisho ya kuchukua kinachokufaa kwa kuzingatia ukubwa wa kazi yako, mazingira yako na aina ya kazi yako.