Treni TRL na TAZARA kutumia umeme. Mwendo kasi kama Ulaya

Treni TRL na TAZARA kutumia umeme. Mwendo kasi kama Ulaya

Ubungoubungo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2008
Posts
2,502
Reaction score
741
What are we waiting for, gas tunayo, tunaweza kutengeneza umeme mwingi wa kutumia hadi tukauza nje, kwanini train zetu zisianze kutumia umeme kama Ulaya na tupate zile za faster kama wenzetu?

Nini kinazuia? Na kama kuboresha reli na train wanaosabotage ni wamiliki wa malori, kwanini tusitumie kama Kagame kuwawinda hao tuwateketeze wapinga uchumi wa Tanzania hao?

Au kwasababu malori mengi yanamilikiwa na watu walioko kwenye system hivyo umasikini wetu ni nafasi yao kuendelea kuwa matajiri? Hadi lini na kila kitu tunacho, Mungu atupe nini jamani, gunia la chawa tujikune au upele?
 
Mkuu badilisha heading ya story yako, namna ulivyoandika ni kama vile wahusika/serikali imesema mradi upo kwenye pipeline kumbe unatoa mawazo tu kuwa kitu hicho kinawezekana kwa resources tulizonazo.
 
Labda hawa wezi wanaoficha pesa Uswis
wafungwe wote.
 
tram toka kibamba hadi posta, mbona itakua safi sana! sidhani kama inashindikana.
 
tusubiri kenya wajenge ili na sisi tuige, manake sisi wenyewe kuanza si rahisi akili zetu zinahitaji kustuliwa kidogo..hahaha. ila ningekuwa nimeshika rungu, hakika ningeleta mabadiliko makubwa sana kwenye bandari, reli na viwanja vya ndege na kwa kutumia hivyo tu nchi yangu Tanzania ingeendelea. Mungu ibariki Tanzania.
 
Naona unaanza kuwa na ahadi za JK.Hilo haliwezekani chini ya serikali ya CCM.sehemu kubwa ya wana CCM ni wale waliotengezwa na siasa za CCM,hawajawahi hata kufanya kazi kwenye Private firms,waliofanya kazi serikalini walibewa kuelekea huko na mwisho wanarudi kukitumikia chama e.g Mwigulu.Ni lazima waje watu wenye mawazo mapya wanaoona inawezekana.
 
tupo kwenye mchakato na tuko katika hatua za mwishomwisho za utekelezaji. tutaanza na Tazara na ndio maana tumeamua kufukuza wafanyakazi wote wa zamani ambao ni analogy ili tuingize wapya yaani digital watakaoweza kuendesha mitambo ya treni ya kutumia umeme! nadhani watanzania mtatuunga mkono katika hili maana tumechoka sasa! kila siku migomo! tumechoka...wafukuzwe tu!.
what are we waiting for, gas tunayo, tunaweza kutengeneza umeme mwingi wa kutumia hadi tukauza nje, kwanini train zetu zisianze kutumia umeme kama ulaya na tupate zile za faster kama wenzetu? nini kinazuia? na kama kuboresha reli na train wanaosabotegi ni wamiliki wa malori, kwanini tusitumie kama kagame kuwawinda hao tuwateketeze wapinga uchumi wa tz hao? au kwasababu malori mengi yanamilikiwa na watu walioko kwenye system hivyo umasikini wetu ni nafasi yao kuendelea kuwa matajiri? hadi lini na kila kitu tunacho, Mungu atupe nini jamani, gunia la chawa tujikune? au upele?
 
Back
Top Bottom