Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Juzi Alhamisi abiria waliokuwa wakienda kaskazini walilazwa njiani wilayani Same bila kuambiwa sababu, na abiria waliokuwa waondoke Arusha walilalamika kushindishwa stesheni bila kuambiwa sababu za msingi. Haya matukio mawili yanatokea baada ya shirika la reli kutangaza kuongeza mabehewa sawa na idadi ya mwanzo! Je, kuna wsfanyakazi wa TRC kwa kushirikiana na wenye mabasi ya kaskazini wameamua kulihujumu shirika ili mabasi yapate abiria wengi kwa mtindo uliozoweleka wa kuzidisha nauli?