Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 620
- 1,240
Kwa mara ya kwanza toka tanganyika na Zanzibar kuungana na kupatikana Tanzania Jana safari ya Kwanza ya treni ya umeme ya kisasa yenye kazi ya kusafirisha abiria ambayo inaitwa Electric multiple Unit kwa jina maarufu ni Treni ya mchongoko.
Ilianza safari toka Dar Es salaam, Morogoro mpaka Dodoma. Safari yake ya kwanza imeanza muda wa saa mbili asubuhi na kufika dodoma majira ya saa Tano na kupokelewa na mkuu wa mkoa dodoma mhe Rosemary senyamule.
Treni hiyo yenye Uwezo wa kusafirisha abiria jumla ya 589 lakini waliofanikiwa kusafiri Leo ni 320 ni mashuhuda wa Kwanza kupanda treni ya mwendokasi.
Chanzo: Trc (shirika la reli Tanzania)