TREVO: Je ni kweli inafanya kazi au ni utapeli?

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Habarini wana JF

Kwanza kabisa natambua kuwa Tiba yoyote ile ni imani lakini sio imani tuu lazima na tiba ifanye kaZi

Kwasasa hasa hapa nchini kwetu Tanzania kumekuwa na Tiba asilia nyingi sanaaaa hadi unashindwa kujua ipi ni ipi hasa hii ya watu kujitangazia Tiba zao

Kwasasa TREVO naona inashika kasi sana lakini kiupande wangu nasikia shuhuda tuu toka kwa wauzaji na wahamasishaji wa hii Tiba nashindw kuelewa kama kweli inafnya kazi kama vile navo ambiwa

Nambiwa ni virutubisho na sio dawa lakini shuhuda nazo pata naona watu wanapona magonjwa ambayo ni very very complicated hadi najisemea mwenyewe kama mtu anasimulia kuwa mtu mwenye cancer ambayo ipo stage kubwa kapona sa serikali inasubiri nini kugawa dawa hii kwa wagonjwa

Napata shuhuda za magonjwa makubwa makubwa kabisa na naambiwa kopo moja la TREVO NI laki moja na 80 hadi na 95!

Swali langu ni je kweli hii TREVO inafanya kazi kama vile inavotangazwa au ni propaganda za kumuibia Mtanzania?

Kama kuna mtu hapa alikuwa na mgonjwa wake atwambie kama alipona kwa TREVO

sipo hapa kuwaharibia ila nikutaka kupata ukweli ili tuwasaidie na wengine!
 
Endelea kufanya uchunguzi ili nasisi tupate taarifa vizuri maana utapeli umeshika kasi bongo land.
 

Zaidi ya utapeli
Wizi tuuuuu
 
Vile ni virutubisho tu na nyongeza ya madini kama tunayopewa hospitali na maduka ya madawa.
Zina faida kiasi, lakini bei yake haiendani kabisa na faida zake; NI ULANGUZI wa mchana kweupeee.....
 
hakika bei zake ni kichefu chefu.....
 
Mlitakwa iuzwe mia nane eeh?! Nutritional supplement ni ghali all over the world, ndio maana mnashauriwa kula vyema badala ya kulewa vyema
 
Itabidi wahusika Wa Serikali waifuatilie hiyo TREVO kwa ndani zaidi isije kuwa kuna utapeli wa dawa hizo za TREVO Waziri Muhusika atalifanyia kazi ombi lako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…